Ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na watumishi katika kikao chake cha kawaida cha kazi ikiwa lengo kuu la kikao hicho ni kuongea na watumshi wa makao makuu ya Halmashauri ya Jiji la Arusha pamoja na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha hapo jana.
Miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza Mkurugenzi huyo ni pamoja na watumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa bidii na kuongeza mapato ya Halmashauri na kubana matumizi pamoja na kuangalia maslahi ya watumishi.
“Miongoni mwa mwambo yanayozorotesha ufanisi na utendaji katika sehemu ya kazi ni majungu na fitna hivyo nichukue fursa hii pia kuwaasa watumishi wangu kujiweka mbali na vitendo hivyo kwani ni chukizo kwa Mungu na pia mnapaswa kujiwekea mipango maalum katika kufikia malengo yenu” alisema Dr. Madeni
Aidha, Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Ndg. Baltazar Amedeus Ngowi alitoa fursa kwa watumishi kueleza changamoto, matatizo na maoni yao ambapo changamoto kubwa zilizobainishwa na baadhi ya watumishi hao ni ukosefu wa kantini ya chakula hali inayopelekea usumbufu mkubwa kwa wahudumu wa ofisi kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati, ufinyu wa ofisi hasa katika idara ya elimu na motisha ndogo hasa kwa wafanyakazi katika kada za chini ambapo Mkurugenzi aliahidi kuzipokea changamoro hizo na kuzifanyia kazi mara moja.
Kikao hicho kitakuwa ni endelevu katika kila robo ya mwaka ambapo katika vipindi vijavyo Mkurugenzi Dr. Madeni pia atakutana na watumishi wengine katika ngazi za kata pamoja na idara na kada mbalimbali zilizo chini ya Halmashauri ya Jiji la Arusha lengo likiwa ni kufahamiana na kusikiliza kero pamoja na changamoto mbalimbal zinazowakabili watumishi wa Jiji hili.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa