Na Mwandishi wetu.
Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha na Mgeni maalumu Mhe . John Mongella amewaomba viongozi wa kidini na viongozi wa kimila kuendelea kushirikiana na kushikamana na serikali katika kuhakikisha mkoa wa Arusha unakua bora na kuwaahidi kuwa serikali ipo tayari wakati wowote kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa viongozi hao.
Mhe. Mongella Amesema hayo jana alipohudhulia hafla iliyoandaliwa na viongozi wa kimila na viongozi wa kidini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa (AICC) ya kumpongeza Mhe.Rais katika uongozi wake na kazi alizofannya kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
"Haya tunayoyaona katika Jiji la Arusha yametendeka ni pamoja na uongozi uliotukuka wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na maombi yenu, ibada zenu,sala zenu na dua zenu zinamchango mkubwa sana katika kuiweka Arusha kuwa na amani na wa omba tuendelee kushikamana na pale mnapoona tumepungukiwa msisite kutushauri na kutuelekeza tutakua tayari wakati wowote,na ninawahaidi kufikisha salamu kwa Mhe Rais kuwa hakikisha kuwa viongozi wa kidini na viongozi wa kimila wako pamoja na mama Samia". alisema Mkuu huyo.
Naye Shekhe wa Mkoa wa Arusha Ndugu,Shaban Bin Juma amempongeza Mhe. Rais kwa hatua aliyochukua ya kuamua kufanya mazungumzo ya amani na wanasiasa wa vyama tofauti nchini kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo na kupata mawazo ya namna ya kuindesha nchi kwa pamoja na kwa amani.Aidha Shekhe huyo ameufananisha uongozi wa mama Samia na mama Baliqis kwa namna anavyotumia fikra zake kuiokoa nchi yake,mali za wananchi wenzake na maisha ya watu wake.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya amani na mwakilishi wa Jumuiya ya Maridhiano Dr.Solomoni Masamva amemshukuru Mhe.Rais kwa kuwa nguzo ya amani kwa kuliunganisha Taifa la Tanzania kwa pamoja na watu wake lakini pia kuunganisha Taifa na mataifa.Lakini pia katika kuliongoza Taifa katika Janga la uviko19, kwa namna alivyojitoa kuonesha mfano kwa watanzania kwa kuchanja na watanzania kumuunga mkono kwa kuendelea kuchanja.Amemshukuru pia kwa jinsi fedha za uviko 19 zilivyotumika katika kujenga madarasa na hospitali nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoriki na Umoja wa Kanisa Mkoa Arusha(UKAMA) Father Malisa, amemuomba Mhe Samia kuendelea kutekeleza mazuri anayo fanya kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya Taifa,pia amempongeza kwa kufanya filamu ya Royal tour kwani kwa kipindi hiki kifupi tayari imebadilisha maisha ya wana Arusha kutokana na wageni na watalii kuongezeka kwa kasi kwenye Mkoa huu ,pia amemuhakikishia wao kama taasisi ya kidini kutoa ushirikiano kwa serikali katika zoezi la sensa linalotarajia kufanyika agosti mwaka huu kwa kuwahamasisha watu kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wa Kiongozi wa kimila Ndugu Ole Kisongo amesema licha ya mama Samia kuwa ni mchapakazi lakini pia ni mama mwenye upendo na wananchi wake na mpenda amani kwa watu wote na mpenda maendeleo kwa taifa lake,amempongeza kwa kuendelea kudumisha amani ya nchi na mataifa duniani.
Akiongea kwa niaba ya Kamishna wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Bi. Witness Shoo amesema Shirika linampongeza mama Samia katika juhudi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha uhifadhi na utalii uko mbele katika Nchi yetu,ametumia fursa hiyo kueleza jinsi Shirika hilo la Hifadhi ya Taifa ilivyo jiweka tayari kwa ajiri ya kupokea wimbi kubwa la wageni na watalii ikiwa ni matokeo ya filamu ya The Royal tour aliyoifanya Marekani ,amesema Shirika limejipanga katika kuweka miundombinu mizuri kwa ajiri ya usalama wa wageni na kuweka wanyama katika maeneo mazuri na tulivu,pia kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Naye mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanayakazi Tanzania(TUCTA)Ndugu,Tito Cholobi amemshukuru Mhe.Rais kwa kuongeza asilimia 23.3 ya mshahara kwa watumishi wote wa Umma,kwa kuongeza posho kwa watumishi kutoka laki moja na ishirini hadi laki mbili na hamsini ,lakini pia kwa kuongeza posho ya muda wa ziada kutoka elfu 30 mpaka elfu 60,Na pia kwa kuleta mfumo wa kuwapandisha madaraja watumishi,ametumia fursa hiyo kumuombea Mhe.Rais afya njema na nguvu ya kuendelea kuliongoza Taifa,amemuhahidi kwa niaba ya watumishi wote kufanya kazi na kumuunga mkono.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa