Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Arusha umefika tarehe 05/09/2017 na kudumu kwa muda wa siku moja katika Wilaya hii na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Monduli siku iliyofuata ya tarehe 06/09/2017.
Mwenge wa Uhuru ambao ulipokelewa katika eneo la Chekereni uliweza kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uzinduzi wa viwanda, Zahanati, Maji, Mradi wa vijana, barabara, madarasa, mabweni na kutembelea vikundi vya ujasiriamali.
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeendelea kujitengenezea historia baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi saba katika jiji hili yenye thamani ya shilingi bilioni 5 na milioni 500 na kati ya hiyo imetekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani, fedha za maendeleo, Fedha za wahisani pamoja na nguvu za wananchi.
Miradi yote imetekelezwa kwa ubora wa hali ya juu na thamani ya fedha imeonekana na kwa hakika miradi hiyo imeweza kumaliza ama kupunguza kero za wananchi mbalimbali waliokua wakipata shida ya Maji, umbali wa huduma za Afya, ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na ubovu wa Miundominu duni ya kusomea kwa wanafunzi wetu.
Ama kwa Hakika Mwenge ni chachu ya Maendeleo, huleta heshima pale penye dharau, mshikamano penye umoja na hurudisha upendo baina ya watu na watu pale ambapo upendo ulipotoweka.
Asante sana Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 na karibu tena Mwaka 2018.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa