• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Rais Samia amwaga vitabu Jiji la Arusha

Posted on: January 21st, 2022

Na Mwandishi  Wetu,

Arusha.

Halmashauri  ya Jiji la Arusha imepokea zaidi ya vitabu laki moja vya kiada na ziada kwa shule zote za  msingi za serikali zenye mchepuo wa kiingereza na Kiswahili kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba.

Akizungumza mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kwa walimu wakuu wa shule za jijini hapo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima amesema haijwahi kutokea  kwa jiji jilo kupokea idadi kubwa ya vitabu kama ilivyo sasa.

“Hii ni jitihada za Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa nchini, hivyo nawaomba wana Arusha kutambua jitihada hizi na kumuunga mkono, na sisi kama Jiji hatutamuangusha, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii na kwa ari zaidi” Alisema Dkt Pima.

Dkt Pima amesema wamepokea jumla ya vitabu 107,644 ambapo wamevigawa kwa shule zote za msingi zilizopo katika jiji hilo kwa maana ya shule zenye mchepuo wa kiingereza pamoja na zenye mchepuo wa Kiswahili kwa masomo mbalimbali.

Ameongeza kuwa pia vipo vitabu vya miongozo ya walimu, vitabu vya elimu maalum pamoja na vitabu ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) na kwamba tayari ameshatoa maelekezo kwa walimu wakuu wa shule hizo kuvitunza ili viendelee kutumika kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi jiji la Arusha Mwl. Reginald Peter Richard amemuhakikishia Mhe. Rais kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba na kushika nafasi ya kwanza kitaifa kutoka nafasi ya pili walioshika katika matokeo hayo mwaka jana.

“Hili ni deni kwetu, kwani Mhe. Rais ametuwekea mazingira mazuri ya kuhakikisha sekta ya elimu inakua, niseme tu kuwa hata hii nafasi ya pili tulioshika mwaka jana siyo sawa, sisi tulipaswa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwani hatuoni sababu ya kushindwa kutokana na kuwepo kwa miundombinu bora ya elimu” Alisema Mwl Richard.

Amesema moja ya mikakati ya kuhakikisha kuwa jiji hilo linashika nafasi hiyo ni pamoja na kubuni mbinu mbalimbali za ufundishaji zitakazosaidia stadi za KKK, kudhibiti tatizo la utoro na tayari wameshaweka mkakati na wazazi ili wanafunzi waweze kupata chakula cha mchana.

Aidha amesema ameshatoa maelekezo kwa walimu hao kuweka utaratibu wa kuwaazimisha wanafunzi vitabu hivyo ili waweze kujisomea majumbani siku za mwishoni mwa mwiki badala ya kuwaacha kutumia muda huo kucheza.

Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mhe. Maximilian Iraghe amesema licha ya vitabu hivyo kuwasaidia wananfunzi katika masomo yao lakini pia vitatoa motisha kwa walimu katika ufundishaji kwani hapo awali walimu hao walikabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitabu vya miongozo na ufundishaji.

Baadhi ya walimu waliozungumza wakati wa upokeaji wa vitabu hivyo. Mwl. Zebedayo Mollel Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Themi pamoja na Mwl. Zukra Karunde Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Daraja Mbili walisema serikali itegemee mabadiliko makubwa kwenye suala la kitaaluma.

Wamesema awali kitabu kimoja kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya tano lakini kwa idadi ya vitabu walivyopokea kitabu kimoja kitatumiwa na mwanafunzi mmoja au wawili tu. 

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa