• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

RAS Arusha awataka watumishi wa umma kuwahudumia wananchi kwa weledi

Posted on: January 14th, 2022

•Aipongeza Idara ya ardhi kwa kupunguza migogoro ya ardhi

• Mkuu wa Wilaya awapa kongole ukusanyaji wa mapato.


Na Mwandishi Wetu

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amewataka watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo kutumia busara katika kushughulikia malalamiko ya wananchi ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu na sheria zinazoongoza ushughulikiaji wa malalamiko yao.

Akizungumza katika kikao cha utambulisho wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa watumishi wa Jiji hilo, Dkt Kihamia amesema hata Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatilia mkazo suala la kuwahudumia wananchi kwa busara ili kuhakikisha haki inapatikana.

“Kwanza katika kushughulikia malalamiko ya wananchi ni wajibu apokelewe vizuri, asikilizwe vizuri na aelekezwe vizuri, na ndiyo maana tunaambiwa katika kuwahudumia wananchi inapaswa busara itumike kwa asilimia 30, taratibu na sheria inachukua asilimia 70” Alisema Dkt Kihamia.

Kwa upande mwingine Katibu wa Tawala huyo ameipongeza Idara ya ardhi kwa kuendelea kushughulikia vyema migogoro ya ardhi hali iliyopelekea migogoro hiyo kupungua kwa kiasi kikubwa  na kusema hatua hiyo inaonesha Idara imejipanga na inafanya kazi kwa kushirikiana.

Ameongeza kusema ili watumishi waweze kutimiza malengo ya serikali ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi ni lazima kuwepo kwa motisha kutoka kwa wakubwa wao wa kazi, hivyo suala la motisha kwa watumishi ni la muhimu.

Akizungumza na watumishi hao, Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda ameipongoza halmashauri hiyo kwa ukusanyaji wa mapato hali iliyopelekea Jiji hilo kuwa miongoni mwa majiji yanayofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato nchini.

“Siyo kwa upande wa mapato pekee, hata katika Idara nyingine kama vile Afya, Elimu na Mazingira, mmefanya vizuri sana, hivyo ni jambo la kujivunia licha ya kuwa ni lazima tuweke mikakati ya kuboresha zaidi” Alisema Mkuu wa wilaya.

Moja ya mikakati aliyoshauri ni pamoja na kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 23 zinazokusanywa kwa sasa kwa mwaka hadi kufikia shilingi bilioni 30 kwa mwaka.

Na katika kufanikisha mkakati huo ameziagiza Idara za Uchumi na Fedha kufanya zoezi la sensa kwa muda wa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara ili kubaini ni nani anastahili kupita mapato ya halmashauri na ni nani halipi na majibu ya sensa hiyo aipate baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.

Mhe. Mtanda pia amewataka watumishi hao kushirikina na Chama cha Mapinduzi katika kuwahudumia wananchi pamoja na kuzingatia suala la nidhamu na kuheshimiana Miongoni mwao bila kujali vyeo na madaraja waliyonayo ili kuleta nguvu katika kuisaidia serikali kuwahudumia wananchi wake.

Awali akimkaribisha mkuu huyo wa wilaya, Mkurugenzi  wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima amemuhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa ofisi yake itampa ushrikiano wa kutosha kwa kuwa wanafanya kazi kama timu moja.

Dkt. Pima amesema wao katika kutimiza majukumu yao wanazingatia kauli mbiu inayowaongoza ya *“kutoa huduma bora kwa wananchi ili kutimiza malengo ya serikali”* na ndiyo sababu wameweza kukusanya mapato kwa kiwango kikubwa.

"Sisi Jiji tutakupa ushirikiano wa kutosha, na kwa kuwa tunafanya Kazi kwa timu, hili litawezekana kwani hata haya mapato kupanda ni kutokana na kufanya Kazi kwa ushirikiano kama timu moja" alisema Dkt Pima.

Mhe. Said Mtanda 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha

Dkt. John Pima 

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha

Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa