MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amesema Ujenzi wa miundo mbinu bora ya Biashara katika maeneo ya masoko ni jambo la muhimu na kwamba ni lazima ijengwe miundo mbinu bora yenye uwezo wa kuishi miaka 50 ijayo.
Mh. Mongela amesema masoko katika Jiji la Arusha yamepitwa na wakati kwamba suluhisho pekee ni kujenga masoko ya kisasa yatakayowezesha Wafanyabiashara kufanya Biashara kwa nafasi na kulipa kodi zao hatimaye kuongeza kipato na kuchangia uchumi wa nchi kwa kulipa kodi.
Akizungumza mara baada ya kusikiliza kero za wananchi Tarafa ya Themi katika Kata ya Levolosi eneo la Kilombero alisema kuwa malengo ya Ujenzi wa miundo mbinu bora yatafikiwa kwa ushirikiano baina ya viongozi kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anapenda Umoja na Viongozi wa Mkoa wa Arusha wana umoja na watafikia matarajio yao.
Mhe. Mongela akizungumzia suala la Wamachinga alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa Wafanyabiashara hao na kuwa watajadili kwa pamoja nakufikia suluhu ya jinsi yakutatua changamoto zao kwamba mazingira bora na sahihi ya biashara ni muhimu kwa kila mtu.
Katika hatua nyingine amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwa kwa wananchi wote wa Mkoa wa Arusha na Jiji la Arusha kwa kuwa ulinzi na usalama ni matokeo ya mafanikio kwa wananchi wote.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa