• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Rc Gambo ateta na Watendaji wa Kata, Mitaa kuhusu kodi ya Majengo

Posted on: April 5th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na watumishi wa Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa kukusanya Tsh Bilioni moja za kodi ya majengo kwa kipindi cha Mwezi wa Nne.

Rc Gambo ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na watendaji wa Kata, Mitaa, Wahasibu wa Mapato, wataalamu wa Mipango Miji pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Arusha kilichofanyika mapema wiki hii.

Akizungumza katika Kikao hicho cha kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto ya kutokusanyika kwa Kodi ya Majengo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 Rc Gambo amesema hata kama hata kama chanzo hicho kimehamishiwa TRA, Halmashauri ya Jiji bado ina mchango mkubwa katika kufikia Malengo yaliyowekwa kwa kushirikiana na wataalamu wa TRA kwenye  Kata na Mitaa yote ya Jiji.

Aliongeza kuwa Jiji kuna watumishi wengi ambao wanafahamu kila nyumba katika mitaa yote ya Jiji na wamekuwa wakifanya kazi hii kwa kipindi kirefu hivyo wana uzoefu wa kutosha na ushiriki wao katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka wa Fedha ni muhimu sana ili kwa pamoja tuweze kufanikiwa kukusanya maduhuli ya Serikali kwa ufanisi.

Alisema maeneo yote ambayo hayajapimwa kila mmiliki wa jingo atalipia Tsh 15,000 na maeneo ambayo hayajapimwa ila yamefanyiwa Uthamini watalipa kwa kiwango walichokadiriwa na kwa maeneo yaliyopimwa ya kwa viwango vya juu tunaangalia utaratibu mzuri wa kukusanya hivyo kila mmiliki wa jingo atomize wajibu wake kwa kulipa kodi hii.

“Hapa tunachohitaji ni kuunganisha nguvu ya pamoja ili tuweze kufikia Malengo na sio kwa sababu Chanzo hiki kiko chini ya TRA kwa sasa basi Jiji basi Taasisi zingine zisitoe Ushirikiano mimi kama Msimamizi wa shughuli za Serikali ntashirikisha kila Taasisi inayohusika ili kufanikisha Malengo ya ukusanyaji na sio katika chanzo hiki tu bali katika Vyanzo vyote alisema Gambo”.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kazi hiyo itafanyika kwa kadiri ya Maelekezo waliyoyapokea na kwamba ana imani kubwa na wataalamu wa Jiji kwa kuwa wamekwishashiriki mazoezi  kazi mbalimbali na kuleta mafanikio makubwa katika Wilaya hii.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha bwana. Athumani J. Kihamia aliongeza kuwa atawasimamia watendaji ipasavyo katika kukusanya kodi ya Majengo na ataendelea  kuwajengea uwezo  ili kuongeza ufanisi katika zoezi hilo.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Arusha, bwana Apili Mbarouk ameelezea hali ya ukusanyaji wa chanzo hiki kwamba hairidhishi kwani mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya Tsh Mil 200 tu wakati malengo ya Ukusanyaji wa mwaka wa Fedha unaoishia Juni 2017 ni Tsh Bil 5 hivyo ni vyema kuongeza nguvu ili kufikia Malengo.

 Kikao kazi hiki ni muendelezo wa wa Vikao vinavyoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo katika kutatua kwa pamoja changamoto za sekta mbalimbali katika Mkoa huu ili kuleta Mafaniko ya pamoja

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa