Ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na watumishi wa Jiji la Arusha kufuatia agizo na msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli juu ya suala zima la ulipaji wa kodi na ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ndio muhimili mkuwa wa Taifa letu.
Mkuu wa Mkoa pia katika kikao chake na watumishi wa Jiji la Arusha kilichofanyika hapo jana ameagiza watumishi kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa fedha wa ndani na nje katika kuwasilisha taarifa muhimu za matumizi ili kukwepa hoja zisizo za msingi.
Pia miongoni mwa mambo aliyoyatilia msisitizo ni pamoja na suala la baadhi ya watumishi kutowabugudhi wafanyabiashara wadogo almaarufu kama machinga kama agizo la Rais linavyosema badala yake kama serikali tunawajibika kuwatengenezea mazingira rafiki na uhuru karika shughuli zao za kujiingizia kipato na sio kusimama kama kikwazo.
Kadhalika, aliwaonya mawakala wa ukusanyaji taka katika Jiji la Arusha kuacha kuwabugudhi wamiliki wa viwanda katika jiji hili kwa kukusanya tozo ama faini zisizo za lazima kwani wamiliki hao wa viwanda wamekuwa ni chachu ya kusogeza gurudumu la maendeleo katika jiji letu hivyo amewaagiza watumishi idara ya Usafishaji na Mazingira kulisimamia hilo.
“Kwa mfano mmiliki wa kiwanda cha Mount Meru Millers, mfanyabiashara huyu ni mdau mkubwa katika maendeleo ya elimu jijini hapa na amejitolea kufanikisha lishe ya kila siku kwa zaidi ya wanafunzi 20,000 kwa shule za msingi katika Jiji hili hivyo hapaswi kutozwa faini zisizo za kisheria na mawakala wachache wenye kutaka kuharibu sifa nzuri ya Jiji letu” alisema mkuu wa mkoa
Pia amewaagiza maafisa utumishi katika Halmashauri kutokuwa kikwazo kwa watumishi kupanda madaraja badala yake wasimamie maslahi ya watumishi ikiwemo kutatua changamoto ya upishanaji wa mishahara watumishi wanaopanda madaraja kwani kwa kutofanya hivyo kunashusha morali ya watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Changamoto nyingine iliyobainishwa na Mkuu wa Mkoa huyo pia ni ukosefu wa matundu ya vyoo hasa katika shule za sekondari za kata ikiwemo shule ya Sekondari Mkonoo kata ya Terrat, mazingira ya vyoo vya walimu ni mabovu hivyo watumishi mnapaswa kulisimamia hilo na kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wanaojitokeza kutatua changamoto hizo.
Pia amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Richard Kwitega na kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni kutengeneza mpango mkakati kuhakikisha maeneo ya ardhi yanapimwa na wananchi kupatiwa hati miliki zao na watumishi wapewe kipaumbele katika kupatiwa viwanja vinayouzwa ikiwemo vya Mateves na Suye kwa mikopo yenye riba nafuu.
“Katika upande wa afya serikali inajenga vituo vikubwa vya afya katika jiji la arusha ikiwemo kituo cha afya Murret ambapo nichukue fursa hii kumpongeza Eng. Samuel Mshuza, Kaimu Mhandisi wa Jiji kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho. Pia tunajenga hospitali za wilaya kwa mkoa mzima ambapo kwa Jiji la Arusha ujenzi wa hospitali ya wilaya iliyopo katika kata ya Engutoto ipo katika hatua za umaliziaji” alisema Mkuu wa Mkoa.
Alimaliza kikao chake wa kuwahimiza watumishi kujiimarisha katika maandalizi ya Mwenge ambapo kwa Jiji la Arusha tunatarajia kuupokea Tarehe 18/09/2019 na ametilia mkazo upewe heshima inayostahiki.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa