Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewapongeza na kuwataka wakuu wapya wa Wilaya za Arusha na Karatu kushirikiana na wananchi, viongozi wa dini, Mila, Chama Cha Mapinduzi na Vyama vingine vya Siasa ili kurahisisha utendaji wa majukumu yao.
Mhe. Mongella ametoa pongezi na rai hayo alipokua akizungumza na Wakuu hao Wilaya na wageni waalikwa walio hudhuria tukio la kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba na ukaribisho wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
"Wakati Mwingine viongozi hujisahau na Kufikiri tunajua sana kuliko wananchi, wanauelewa wakutosha ndiomaana wanaendesha maisha yao, ukichanganya na ujuzi wako na utakaowakuta kule liko jambo la maana litafanyika" - Mhe. Mongella
Aidha Mhe. Mongella ameeleza kua ni muhimu kushirikiana na makundi hayo muhimu ili kuleta ufanisi katika kazi, akitolea mfano Viongozi wa Dini na wa kimila ambapo ameeleza kua serikali imefanikiwa kugawa Chanjo za UVIKO-19 50,000 kwa awamu ya kwanza na chanjo 33,500 kwa awamu ya pili ambapo hadi sasa wamefikia zaidi ya 80% huku wakitegemea kupokea zingine.
Kwa upande wake Mhe. Mtanda amemshukuru Mhe. Rais SSH, ameahidi kua muaminifu na kuomba ushirikiano kwa viongozi wenzake na Wananchi wa Arusha na kuahidi kusimamia zoezi la ukamilishwaji wa vyumba vya madarasa ifikapo 15/12/2021, kulisimamia swala la wafanyabiashara wadogo wadogo na kusimamia usafi wa mazingira na utunzaji wa mji.
Uapisho huo umefuata baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufanya teuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa wilaya ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa Sasa Mhe. Said Mtanda alikua Mkuu wa wilaya ya Moshi, huku Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas Kanyanda akihamia Moshi, na Mhe.Dadi Kolimba kuteuliwa kua mkuu wa Wilaya ya Karatu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa