Na Mwandishi wetu
SERIKALI imesema kuwa itawezesha vijana kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki wa njia ya kisasa ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwawezesha kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana na kwamba wadau wa ufugaji wenye nia yakufundisha vijana kupata ujuzi wa ufugaji wa kisasa watapewa ushirikiano wa karibu ili waweze kufanikisha nia njema ya kuwapatia vijana ujuzi kwa kushirikiana na serikali .
Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Mh Pauline Philipo Gekul akizungumza katika kituo na shamba la uzalishaji Samaki wa njia ya kisasa kinachojulikana kwa jina la Shanzan kilichopo Njiro ,Halmashauri ya Jiji la Arusha alisema kuwa mikopo wa Vijana inayotolewa katika Halmashauri wa asilimia 4 inatakiwa kutumiwa kuanzisha mradi kama huo wa ya ufugaji wa samaki wa kisasa .
Mh Gekul alitaka vijana kujitokeza kuchangamkia fursa ya ufugaji kwamba Serikali inania ya kuongeza ajira kwa vijana kuwa ufugaji ni njia mojawapo ya kuajiri Vijana .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima alisema kuwa tayari Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza mkakati wa ufugaji wa kisasa na kwamba mikopo ya makundi maalum ya vijana ,wanawake na walemavu itaanzisha miradi mikubwa kama ufugaji wa kisasa wa Samaki na kuhimiza makundi hayo kujitokeza ili kupatiwa elimu na fedha za kuanzisha miradi hiyo .
Dk.Pima anasema kuwa kuwa tayari Tshs zaidi million 500 zipo kwa ajili ya kukopesha makundi maalum ya Halmashauri hiyo na kuhimiza Vijana kujitokeza wakiwa wamejiunga kwenye vikundi na kuandaa mpango bora wa mradi husika ili kuweza kupata mkopo wa kuanzisha ufugaji bora utakaowaondolea umaskini.
“Sasa hivi hatutoa fedha ,tutatoa fedha kwa ajili ya miradi na vifaa ,niwaombe makundi maalum kuja na mpango bora kuibua mradi wanaodhani utawawezesha kufikia malengo ya mafanikio “alisema Dk.Pima
Naye ,Naibu Meya wa Jiji la Arusha Mh. Veronika Hosea akizungumzia mradi huo alisema kuwa kwa kushirikiana na madiwani wenzake ,watahakikisha wanahamasisha ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa kwa kuwa unaweza kufuga hata nyumbani na siyo lazima katika mabwawa ya samaki .
Mh. Hosea anasema kuwa Jiji la Arusha linajivunia kuwa na mfugaji wa samaki wa njia ya kisasa kama huyo kwamba atafundisha vijana na watu wenye nia ya kufuga kwa kisasa .
Zainali Bhimani ,ambaye ni mwekezaji wa wa Shamba la Samaki Shanzan Njiro ,anamuomba Naibu Waziri kumpelekea ombi la kusafirisha samaki kwenda maeneo mbali mbali nchini kwa bei nafuu kwa kuwa gharama za usafirishaji ni kubwa hali inayomfanya kushindwa kufikia malengo yake kwa haraka .
Bhimani aliongeza usafiri wa gari unachelewesha kufikisha mzigo haraka hali inayochangia samaki kuharibika kwamba usafiri utamuwezesha kufikia walengwa wengi hatimaye kuwezesha kuchangia uchumi wa nchi .
Pamoja na mambo mengine alisema kuwa yuko tayari kufundisha makundi mbali mbali namna ya ufugaji bora wa samaki kwa njia ya kisasa ambayo haitegemei mabwawa .
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa