Na Mwandishi Wetu
Arusha.
Serikali imesema itaendelea kutekeleza Wajibu wa kuimarisha huduma za chanjo zinazotolewa kwa watoto kupitia vituo vinavyotoa huduma za Afya hapa nchini .
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya chanjo Duniani inayotolewa kwa watoto walio na umri wa Chini ya Miaka 5 (Mitano) katika Halmashauri ya Jiji la Arusha yaliyozinduliwa katika kituo Cha afya levolosi cha Jijini humo.
Mhe. Mtahengerwa amesema Serikali imeendelea kutoa elimu ya afya kuhusiana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa njia mbali mbali ikiwemo vyombo vya habari na vituo vya kutoa huduma za Afya.
Mtahengerwa ameeleza kuwa Mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa maisha yake na Kwa jamii inayomzunguka kwani anaweza kuambukizwa au kuambukiza mwingine ugonjwa pasipokuwa na kinga na kuongeza kuwa Chanjo hizo ni salama na hutolewa bila malipo na wauguzi wenye ujuzi .
"Chanjo zitolewazo katika zoezi hili ni zilezile ambazo hutolewa kwenye vituo vya huduma ya Afya katika ratiba ya kawaida ya utoaji wa huduma ya chanjo "alisema Mtahengerwa.
Sambamba na hayo amesema Halmashauri ya Jiji la Arusha inaendelea kutoa elimu ya afya kwa umma na huduma mbali mbali za tiba na kinga kwa kufuata miongozo yote ya Wizara ya Afya na mwitikio ni mkubwa kwa jamii.
Naye Dkt. Samson Joseph, ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha ameeleza umuhimu wa chanjo kuwa ni pamoja na watoto kujikinga pindi wanapopata magonjwa kutodhurika Kama mtoto mwingne ambaye hajapata chanjo.
"Kuna magonjwa mengine Kama surua tayari mtoto anapokuwa na chanjo anapokumbana na ugonjwa Kama huu kwakweli anaweza hata dhurika Kama mtoto mwingine ambaye hajapata " alisema Dkt. Joseph.
Aidha kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya chanjo Duniani Ni "jamii iliyopata chanjo, jamii yenye Afya" ambapo kitaifa yamezinduliwa mjini Babati Mkoani Manyara.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa