Wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha wanafuatilia masomo yao kwa kujua wanafundishwa nini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda alipokuwa akikagua shule ya awali ya NAFCO iliyopo katika kata ya Olmoti, Jijini Arusha.
Aidha, amesisitiza zaidi kwa wazazi kusimamia maadili ya Watoto wao kwani Dunia imebadilika sana, kwa kufanya hivyo kutasaidia kubaini mmomonyoko wa maadili mapema na kuwarekebisha.
Vilevile, amewataka wananchi hao wa kata ya Olmoti kushiriki katika vikao vya vijiji ili waweze kujua maendeleo ya vijiji vyao kwa kupanga mipango kwa pamoja.
Amewataka wananchi hao kuendelea kumuunga Mkono Rais Dkt.Samia kwani amefanikisha kuwasogezea shule karibu baada ya Watoto wengi kutembea umbali wa Kilometa 7 kila siku kuifuata shule.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda amefanya ziara ya siku Moja katika Jiji la Arusha kwa kukagua Miradi ya Maendeleo na kutatua kero za wananchi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa