Watumishi wa afya wametakiwa kuhakikisha wanatoa huduma Bora na lugha nzuri kwa wananchi.
Hayo, yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI anaeshughulikia afya, ustawi wa jamii na lishe Dkt. Wilson Mahera alipokuwa akizungumza na watumishi wa afya katika Kituo cha afya Levolosi.
Amesema, Serikali imeboresha miundombinu ya afya kwa kuongeza Zahanati na Vituo vya afya kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya nchi ilikuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora na zauhakika.
"Hakikisheni mnatoa huduma inayojali kwa wananchi, hii itawasaidia kubaini maboresho yaliyofanywa na Serikali yao".
Ameitaka Halmashauri kupitia timu ya usimamizi wa huduma za afya (CHMT) kusimamia maadili ya watumishi wa afya na kuchukua hatua kali kwa wale watakaoenda kinyume.
Pia, amesisitiza usimamizi mzuri wa dawa zilizopo zitumike vizuri kwa manufaa ya wananchi .
Vile vile, amewataka watumishi hao kusimamia matumizi sahihi ya makusanyo katika Kituo hicho ili ziweze kusaidia katika kuboresha zaidi huduma za afya.
Dkt.Mahera amelekeza Elimu itolewe zaidi kwa wakinamama wajazito kuhudhuria kliniki kadri inavyotakiwa ili waweze kujifungulia katika Vituo vya afya.
Ziara ya Dkt. Mahera imefanyika katika Jiji la Arusha kwa kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha afya Levolosi na alizungumza na watumishi wa Kituo hicho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa