Timu ya wakaguzi wa mradi wa Kuimalisha elimu Sekondari (SEQUIP) kutoka OR-TAMISEMI,Wizara ya Elimu na Benk ya Dunia wameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa SEQUIP katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumza kwa niaba ya timu nzima,Yusufu Omary kutoka TAMISEMI amesema miradi karibua yote imetekelezwa katika kiwango kizuri.
Maboresho madogo yaliyopo yamaliziwe haraka na wananchi waendelee kunufaika na miradi hiyo.
Aidha, amesema kitendo cha Halmashauri kuongeza fedha katika miradi hiyo ili ikamilike nikitendo cha kuigwa katika maeneo mengine.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Fred Nkya amesema jitihadi zilizofanyika katika miradi hiyo zinaridhisha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa