Uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa 10 Jimbo la Arusha mjini watangazwa,vyama vyajitokeza kushiriki
Na Mwandishi wetu
MSIMAMIZI wa uchaguzi wa Jimbo la Arusha mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima ametangaza tarehe ya uchaguzi wa Wenyeviti wa mitaa 10 ambayo iko wazi baada ya wenyeviti wa mitaa hiyo kuchaguliwa kuwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na wengine kufariki dunia.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Dk.Pima alisema kuwa waliokuwa wenyeviti wa mitaa wapatao nane (8) waligombea nafasi ya udiwani na kushinda na hivyo nafasi zao kuwa wazi na wenyeti wawili walifariki dunia na kwamba nafasi hizo ziko wazi kwamba uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utafanyika Julai Mosi mwaka 2021.
Alisema kuwa wenyeviti hao walichaguliwa mwaka 2019 na kuwa baada ya nafasi kuwa wazi sheria haina budi kufutwa na kwamba sheria ya serikali za mitaa kifungu 44 (1) (2) inaeleza bayana kuwa nafasi zikiwa wazi lazima uchaguzi urudiwe kujaza nafasi hizo.
Alitaja mitaa hiyo kuwa ni mtaa wa Goliondoi kata ya Sekei, Olmatejo B kata ya Sakina, Kwa mrefu kata ya Baraa ,Kirika B kata ya Osunyai JR.
Nyingine ni Olkung’u na Erangau kata ya Terrat, Darajani kata ya Ungalimited, Saccon kata ya Elerai, Block C kata ya Engutoto na Olmokeo kata ya Sinoni .
Dk.Pima anasema kuwa uchaguzi huo ni kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha kanuni za uchaguzi za wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kamati za mtaa katika mamlaka ya wa serikali za mitaa ambapo kifungu hicho kinamtaka Msimamizi wa uchaguzi kutangaza siku 62 uchaguzi huo kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Dk.Pima anafafanua kuwa tarehe 10 Mei 2021 wateteuliwa maafisa ambao watasimamia zoezi zima la kuandaa orodha ya wapiga kura katika maeneo ya mitaa 10 na wataapishwa tarehe 11 na tarehe 12 Mei 2021 watafanyiwa mafunzo ya namna ya kusimamia uchaguzi huo.
Alisema zoezi la uandikishwaji katika daftari la kupiga kura litaanza mara ya mafunzo ya maafisa na uandikishwaji utakuwa unafanyika kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni na itaanza mwezi Mei, 202.
“Wapiga kura ni wakazi wa mtaa husika na watakiwa wawe na sifa zifuatazo, awe ni Raia wa Tanzania Tanzania , awe miaka wa miaka 18 na zaidi awe hana ugonjwa wa akili, awe amejiandikisha kupiga kura na zoezi la uandikishaji na kupiga kura litafanyika katika maeneo ya vituo vilivyotumika mwaka 2019 katika uchaguzi huo. “anasema Dk.Pima.
Dk.Pima anasema tayari vyama 11 vimejitokeza kushiriki uchaguzi huo na kwamba matangazo yataendelea kutolewa kuhamasisha watu wenye nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa kujitokeza ikiwa ni haki ya msingi ya kila mtu.
Pamoja na mambo mengine alieleza Sifa za wagombea kuwa ni awe na umri wa miaka 21 au zaidi na uwezo wa kusoma na kuandika, awe na shughuli inayomuwezesha kuendesha maisha, awe amedhaminiwa na chama husika na awe pia ni mwanachama wa chama anachogombea nafasi hiyo na awe mwanachama na amedhaminiwa na chama hicho husika, awe hana kosa la jinai.
Aliwataka wagombea na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao hatimaye uchaguzi huo uweze kufanikiwa na kuwapatia wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi aliwahakikishia viongozi wa kisiasa na wananchi kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani ambapo amewataka Viongozi wa kisiasa kuepuka lugha za matusi na kashfa wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi huo.
Mh.Kenan aliwataka viongozi wa kisiasa kuwa mstari wa mbele kulinda amani kwa kuhakikisha kuwa kampeni zinafanyika kwa ustaarabu bila kuharibiana na kuvunjiana heshima miongoni mwa wagombea.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa