Halmashauri ya Jiji la Arusha ni miongoni mwa halmashauri zote nchini zinazotekeleza kampeni ya chanjo Surua Rubella pamoja na chanjo ya polio kitaifa inayotolewa kwa njia ya sindano (IPV). Kampeni hii imezinduliwa mapema leo Tarehe 17 Octoba 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Mhe.Gabriel Fabian Daqarro katika kituo cha afya Levolosi ambapo kampeni hii itaeendelea hadi Tarehe 21 Octoba 2019.
Daqarro ameelezea umuhimu wa chanjo ya Surua Rubella na ugonjwa wa Polio ni pamoja na kuwaepushia watoto ulemavu na vifo. Chanjo hii ya Surua Rubella inatolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9-59 ikiwa lengo ni kufikia watoto 51366 na 35966 kwa chanjo ya ugonjwa wa polio. Daqarro amesisitiza timu ya uendeshaji wa huduma za afya wapeleke ujumbe kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa chanjo hizi kwani kampeni hii hufanyika mara baada ya miaka mitano lengo ni kuhakikisha kila mototo aliyezaliwa asipatwe na ugonwa wa surua wala Polio.
“Taifa ambalo linaugua au kuandamwa na magonjwa haliwezi kuzalisha na miongoni mwa maadui aliowataja baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni pamoja na adui maradhi hivyo tukiwakinga leo watoto wetu na magonjwa haya tutakuwa tumelihakikishia taifa letu kizazi chenye afya timamu ambao wapo tayari kufanya kazi kwa bidii iliwaweze kuletea maendeleo kwa taifa letu” Alisema Mhe.Daqarro
Akitoa takwimu ya chanjo ya Wilaya ya Arusha mganga mkuu wa Jiji la Arusha daktari Simon Chacha alieleza kuwa hali ya utoaji chanjo ya Surua Rubella kwa mwaka 2018/2019 ni kwa asilimia 147 zaidi ya lengo la kitaifa asilimia 95 na kwa upande wa chanjo ya ugonjwa wa polio ya sindano (IPV) ikiwa ni asilimia 97 zaidi ya lengo la kitaifa asilimia 95. Hii ni kwa sababu Jiji la Arusha limetoa huduma ya chanjo nje ya wakazi wake kwani watu kutoka wilaya nyingine wamepatiwa huduma hiyo pia.
Mhe. Daqarro ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuimarisha huduma za afya kuanzia miundombinu kwa kuleta vituo vya afya na zahanati karibu na wananchi,upatikanaji wa dawa za muhimu nao umefanikiwa kwa kiwango cha asilimia 98 pamoja na kuimarishwa kwa maslahi ya watumishi .
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa