‘’Jiongeze tuwavushe salama” ni Kampeni ya kuongeza uwajibikaji katika kupunguza /kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vile vya watoto wachanga ambapo kitaifa ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba mwaka 2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na katika mkoa wa Arusha ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo.
Uzinduzi huo wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama umefanyika mapema leo Tarehe 16/07/2019 katika ukumbi wa Golden Rose ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro.
Katika uzinduzi wa kampeni hiyo Mhe. Daqarro alisisitiza ushirikiano wa wataalamu wote katika ngazi ya wilaya ya Arusha na jamii ipatiwe elimu ya kutosha ili kuleta matokeo chanya ya kampeni husika ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
“ Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2015-2016 vifo vitokanavyo na uzazi kwa kina mama ni 556 kati ya vizazi hai 100,000 kiwango hiki ni kikubwa ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo vifo vya wanawake ilikuwa ni 452 na kwa upande wa watoto ni vifo 34 kati ya vizazi hai 1000 ukilinganisha na miaka iliyopita ilikuwa ni vifo 25”alisema Mhe. Daqarro
Naye Mganga Mkuu wa jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha alieleza sababu zinazo pelekea vifo vya uzazi kwa kina mama na watoto wa changa ni pamoja na Ucheleweshaji wa mama wajawazito ngazi ya Jamii unaotokana na baadhi ya mambo kama Mila na Desturi katika jamii mfano kujifungulia majumbani.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa