Katibu tawala wa wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakaposa leo Tarehe 28/01/2020 amezindua kampeni ya mabadiliko ya tabia Nchi kwenye nyanja za usafi wa mazingira. Uzinduzi huo ulidhuriwa na naibu meya Mhe. Paul Matthyesen na Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri ya Jiji la Arusha Ndg. Sifael Kulanga pamoja na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali ikiwemo (SNV) Smart Development Workers ambao ndio wadau wakuuu katika uzinduzi huo uliofanyika Jijini Arusha katika kituo cha afya cha Ngarenaro.
Mhe. mwakiposa akiwa mgeni wa heshima katika uzinduzi huo alisisistiza kwa kusema lengo kuu la kampeni hii ni kutoa elimu kuhusu usafi wa vyoo vyetu na kuhifadhi mazingira kwa ujumla, njia sahihi ya kutoa maji taka na kujenga vituo vya kuwekea taka
Mwakiposa aliendelea kusema mazingira yetu ili yawe salama kuwepo na ushirikiano baina ya afisa afya na mazingira kwa kuwezesha kuvuta maji taka kwenye vyoo kwa njia salama kwa kutumia vifaa kama vile glavu na mabuti kwenye vyoo vilivyo jaa ili kuepusha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu .
Pia alipongeza (smart develompent workers) kwa mchango wao mkubwa kwa kutoa elimu ya utunzaji mazingira kwa jamii na usambazaji wa vifaa vya usafi.
Aliongezea kwa kusema kwenye kampeni hii ya leo ya mabadiliko ya tabia ya Nchi kwenye nyanja ya usafi wa mazingira , Halimashauri ya Jiji la Arusha itatoa ushirikiano wake bega kwa bega kwa kuchimba vyoo shuleni na kuweka sehemu maalumu ya kuwekea taulo za kike na taka zinazozagaa hovyo.
wakati huo shirika la (SNV) linalojishughulisha na kusambaza vifaa kinga vya usafi katika jamii ndani ya Jiji na nje, kuwasaidia walemavu, wanawake wasiojiweza na wajane wanaoishi katika mazingira duni, taasisi hiyo imeshukuru serikali kupitia Halimashauri ya Jiji la Arusha kwa kuunga mkono kampeni hiyo. Nakujitolea kutoa elimu ipasavyo jamii juu ya mabadiliko ya mazingira na kusambaza vifaa popote katika jamii.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa