Afisa afya wa mkoa wa Arusha Bi Vones Uiso amezindua rasmi zoezi la mkakti wa kitaifa wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu waenezao magonjwa leo Tarehe 27 Julai 2019 jijini Arusha . Bi. Vones Uiso akiongozana na Afisa afya wa jiji la Arusha Bw. Allen Sumari,wataalamu pamoja na wadau wengine wameendesha zoezi hili kwa kuanzia kata ya sombetini kisha kata ya moshono ambapo madimbwi na mitaro inayotwamisha maji imenyunyiziwa dawa ya kuuwa viluilui vya wadudu waenezao magonjwa.
Sambamba na hilo Bi. Vones Uiso amesisitiza usafi wamazingira kuzingatiwa katika jamii kwa kuhakikisha taka zote zinakusanywa na kuhifadhiwa kwenye maeneo rasmi yaliyo tengwa kwaajili ya kuhifadhi taka(Jaa). Utaratibu huu utachangia kupunguza mazalia ya mbu na wadudu wanaoenezao magonjwa katika jamii.
Afisa afya wa jiji la Arusha nae amemshukuru mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa kutoa ushirikiano wakutosha kwa idara ya afya na mazingira kwa kuwezesha kupata vitendea kazi na dawa za kutumika katika uzinduzi wa zoezi hilo.
Zoezi la uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu waenezao magonjwa ni zoezi endelevu kwa mikoa yote nchi nzima kwa mujibu wa maelekezo ya wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto.
"Tanzania bila wadudu wadhurifu inawezekana"
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa