• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Vikundi vya Ujasiriamali vyatakiwa kurejesha Mikopo

Posted on: March 9th, 2022

Na Mwandishi Wetu,

Arusha.

Zaidi ya shilingi Milioni mia nne zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vya ujasiriamali 59 kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Arusha fedha zinazotokana na asilimia kumi ya mapato yake ya ndani  kwenye robo ya pili ya mwaka 2021/2022 kwa lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike ambapo amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo ambao ni kutoka kundi la wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili watu wengine waweze kukopa.

Dkt. Mandike amesema kuna dhana potofu imejengeka miongoni mwa jamii kuwa mikopo hiyo ni hisani kwamba haitakiwi kujereshwa hivyo kuwataka wanufaika hao kuondokana nayo na kuhakikisha wanarejesha tena kwa wakati ili kila mtu mwenye sifa anayehitaji mkopo huo aweze kupatiwa.

“Lengo la mikopo hii ni kuhakikisha wananchi wote wenye sifa ya kupata mikopo wanapata kwa lengo la kuwainua kiuchumi, ndiyo maana nasisitiza kuirejesha tena kwa wakati kwani hii mikopo siyo hisani kama baadhi ya watu wanavyodhani” Alisisitiza Dkt Mandike.

Amesema jumla vikundi 32 kutoka kundi la wanawake watapatiwa kiasi cha shilingi milioni 164, vikundi 16 kutoka kundi la vijana nao watapatiwa kiasi cha shilingi milioni 164 pamoja na vikundi 11 kutoka kundi la watu wenye ulemavu watapatiwa kiasi cha shilingi milioni 82.

Mratibu Mwezeshaji kutoka Jiji la Arusha Bw. Loishoki Naju amesema mafunzo hayo yanatokana na sera inavyoelekeza kutoa mafunzo kabla ya kutoa mkopo kwa maana ya namna ya kutumia fedha hizo ikiwa ni pamoja na utunzaji wa kumbukumbu, utafutaji wa msoko, ujasiriamali, ufugaJi bora kwa wale wafugaji, pamoja na kuwakumbusha masuala ya UKIMWI.

Mwakilishi kutoka kundi la watu wenye ulemavu ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho wa vyama vya watu wenye ulemavu Jiji la Arusha Bi. Eunice Urassa amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kujali makundi yote kwenye masuala mbalimbali ikiwemo fursa za kiuchumi na kuwataka wanufaika wenzake kutomuangusha Mhe Rais kwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili waendelee kuaminiwa na kupewa mikopo zaidi.

Halmashauri ya Jiji la Arusha imekuwa kinara wa utoaji wa mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato yake ya ndani ambapo makundi yote kwa maana ya kundi la wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yamekuwa yakipatiwa mikopo hiyo kwa wakati.





Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa