Waandishi wa Habari wapatiwa Elimu ya Ugonjwa wa Malaria
Na Mwandishi wetu
Waandishi wa Habari watakiwa kuandika habari sahihi za Malaria lengo ikiwa ni kuendelea kuelimisha Jamii kuhusu ugonjwa huo na hatimaye kutokomeza ugonjwa na kufikia hatua ya Zero Malaria.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Vones Oiso akizungumza na Waandishi habari katika mafunzo ya kuwajengea Uwezo wa kuandika habari za Malaria alisema aliwataka Waandishi kutambua wanajukumu la kuelimisha Jamii jinsi ya kujikinga na malaria hatimaye kuendelea kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Aliwataka kuwa mabalozi wakuelimisha Umma kuhusu Malaria hususani wiki hii ya kuelekea kilele cha Maadhimisho hayo yatakayofanyika Jijini Arusha tarehe 25 Aprili 2020.
Kwa upande wao wawezeshaji katika mafunzo hayo kwa Waandishi wa habari wakitoa mada kwa nyakati tofauti walisema kuwa lengo la wataalam wa Afya ni kuona Malaria imekoma kabisa kwa kuwa ni ugonjwa hatari usipochukuliwa tahadhari.
Kimsingi walisema kuwa elimu kwa Jamii haina budi kutolewa kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kupitia vipindi Maalum vya kuelimisha Umma kuhusu madhara ya Malaria.
Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa wadudu wanaoneza magonjwa kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii na Watoto Charles Dismas Mwalimu akitoa mada ya udhibiti wa Mbu waenezao malaria kwa njia ya Utangano alisema kuwa Malaria inaweza kudhibitiwa na jukumu hilo ni la kila mtu .
Bw. Dismas alisema kuwa mazingira wanayoishi watu yanapaswa kuwa safi wakati wote na kwamba Waandishi wa Habari na wadau wa Afya wakiwemo wataalam wa Afya wanajukumu la kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa kutunza na kulinda mazingira.
Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali ni maandalizi ya wiki ya kuelekea maadhimisho ya Malaria yatakayofanyika Jijini Arusha katika Uwanja wa Michezo Ngarenaro uliopo Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Pichani : waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vya Habari wakiwa katika mafunzo ya namna ya kukabiliana na Malaria ikiwa ni kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Malaria yatakayofanyika tarehe 25 April, 2021
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa