Wakuu wa Idara Halmashauri ya Jiji la Arusha wapatiwa mafunzo ya Vishikwambi
Na Mwandishi wetu .
Wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wamepatiwa mafunzo ya teknolojia ya mtandao wa jinsi ya kutumia kifaa aina ya Kishikwambi kwa ajili ya kuandikia ,kutumia na kuwekea kumbukumbu za vikao mbali mbali ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama zisizo za lazima za kutumia shajala .
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na yametolewa na wawezeshaji kutoka kitengo cha TEHAMA halmashauri ya Jiji la Arusha.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Msena Bina akizungumza na watumishi hao wakati wa mafunzo aliwataka kutumia ujuzi waliopata kuandaa na kutunza kumbukumbu ipasavyo ili kuwezesha walengwa kupata taarifa kwa wakati .
Pamoja na mambo mengine aliwataka kulinda maadili kwa kutumia vishikwambi hivyo kwa uaminifu na kuepuka kulikisha taarifa kinyume na taratibu kwamba teknolojia hiyo imelenga kurahishia wataalam na wakuu wa idara kazi ya kupata taarifa ,kutuma na kutunza taarifa .
Alisema kuwa Vishikwambi hivyo pia vitatumiwa na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha lengo ikiwa ni kupunguza gharama za kuchapisha taarifa za mikutano ambazo zinatumia gharama kubwa .
Kwa upande wao wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka kitengo cha TEHAMA ambao ni Geofrey Matinya na Innocent Kitauka walihimiza matumizi sahihi ya Vishikwambi na kutoa tahadhari ya kwamba vishkwambi hivyo visipo tumika ipasavyo vianweza leta madhara kwa watumiaji.
‘’Kumbuka kuwa vishikwambi hivi havitakiwi kuwekwa kwenye mifuko ya suruali ,na pia havitakiwi kuingia navyo jikoni ,kwa kuwa ni hatari na vinatumia umeme’’ walisema kwa nyakati tofauti
Walisema kuwa vishikwambi hivyo vikitumiwa kwa makusudi yaliyopangwa ni rahisi katika mawasiliano ,kutoa taarifa na kutunza kumbukumbu .
Teknolojia mpya ya vishikwambi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha itarahisisha utendaji kazi kwa wakuu wa idara na kupeana taarifa za kwa wakati ikiwa ni pamoja kuwapatia madiwani taarifa kwa wakati
………………………………………………………………………………………………………………………
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa