Halmashauri ya Jiji la Arusha imepokea barua ya umiliki wa mradi wa viwanja vya Bondeni City bure pasipo malipo yoyote eneo lenye ukubwa wa ekari 30 lililopo mtaa wa Oloresho Kata ya Olasiti Tarehe 21 Oktoba 2019 ambapo ndipo patakapo jengwa kituo cha kisasa cha mabasi makubwa katika Jiji la Arusha.
katika makabidhiano hayo ya barua hiyo iliyo wasilishwa na timu ya wakurugenzi na wajumbe wa kampuni ya Bondeni Seeds, ndugu Omari Idd Omar mkurugenzi wa kampuni hiyo alieleza kuwa wamekuja kwa lengo la kukamilisha kile walichokuwa wameahidi katika kikao chao, lakini ameambatana na Mkurugenzi mwenzake wa kampuni hiyo ambae nae pia ni muhusika mkuu wa mradi wa viwanja vya Bondeni City anayefahamika kwa jina la Rakesh Yoginder Kumar Vohora ambae ndiye aliyekabidhi barua hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Sifaeli Tuluwene Kulanga.
Timu hiyo iliambatana pia na wajumbe ambao ni Richard Lauye, David Tohuye pamoja na Innocent Mwanga.
Ndugu Sifaeli Kulanga baada ya kupokea barua hiyo ameeleza kuwa watakaa na wataalamu wa idara ya Ardhi mipango miji ili kujadili na kuona kituo hicho cha mabasi kitajengwa upande gani wa eneo hilo ili kubadilisha ''master plan'' ya eneo la mradi wa viwanja vya Bondeni City.
Mwisho
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa