Mwandishi wetu
BALOZI wa Rwanda nchini Tanzania Meja Jenerali, Charles Karamba amewaomba wananchi wa Jiji la Arusha kujenga tabia ya kufanya usafi wa mazingira yao,mara kwa mara ili kuvutia watalii na kuweka taswira nzuri ya nchi kimataifa.
Akizungumza leo Jijini Arusha wakati aliposhirikia shughuli ya usafi,katika eneo la soko kuu na stendi kuu ya mabasi,Meja Jenerali Karamba alisema usafi huweka taswira ya nchi vizuri duniani na kuvutia wengi.
"Wananchi jengeni Tabia ya kufanya usafi mara kwa mara, ukiangalia Arusha ni kitovu cha utalii,hii itasaidia kuweka taswira nzuri ya nchi kimataifa na usafi huepusha uzalishaji wa wadudu wanaoleta magonjwa ya mlipuko,"alisema.
Pia, alisema usafi licha ya kuweka taswira ya nchi vizuri duniani,lakini unasaidia kupunguzia serikali gharama ya kuondoa taka, kwa sababu hakutakuwa na taka nyingi zilizorundikana za kuziondoa.
Aidha, alisema nchini Rwanda wamezoea kufanya usafi kila Ijumaa na mwisho wa mwezi kushiriki na viongozi wao katika shughuli hiyo.
"Kila mmoja anapenda mazingira safi,tukiweka mazingira yetu safi watalii watavutiwa zaidi na kutangaza kwao sifa ya usafi,hivyo tusiache kufanya usafi na sisi tupo tayari kushirikiana katika hili,"alisisitiza.
Alipongeza uwepo wa mahusiano mazuri baina ya nchi hizo na kuwasihi wananchi kushikamana na viongozi wao kwenye mazuri wanayowaelekeza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Saidi Mtanda alishukuru Wanyarwanda, kushiriki katika shughuli ya usafi ambao umefanyika katika kiwango cha kuridhisha.
"Serikali katika kuhakikisha Jiji hili linaendelea kua safi na la kimataifa ukizingatia jiji la kitali, imetoa zaidi ya Sh bilioni 40 kwa ajili ya kujenga soko la kimataifa eneo la Bondeni City na mwezi ujao tenda itatangazwa, ili apatikane mkandarasi na ujenzi uanze,"alisema.
Alisema sambamba na ujenzi huo barabara za lami, soko la Kilombero,Murombo na la machinga katika eneo la stendi hiyo yatajengwa kwa kutumia fedha zaidi ya Sh.bilioni 100 zilizotengwa za mradi wote huo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian alisema Arusha ni lango la utalii kwa sababu watalii wengi wanaofikia nchini hupitia Arusha kwenda kwenye hifadhi mbalimbali,hivyo kujenga tabia ya kufanya usafi kitaipaisha kimataifa mkoa huo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian alisema Arusha ni lango la utalii kwa sababu watalii wengi wanaofikia nchini hupitia Arusha kwenda kwenye hifadhi mbalimbali,hivyo kujenga tabia ya kufanya usafi kitaipaisha kimataifa mkoa huo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Hargeney Chitukuro aliwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi, kushirikiana na Balozi huyo kufanya usafi na kuwaomba kuendeleza tabia hiyo na kukemea watakaowaona wakitupa taka hovyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa