Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewataka wananchi wote wanaoishu maeneo ya mabondeni kuhama mara moja ili kuepuka madhara yanayoweza kuletwa na mvua za Elnino zinazoendelea kunyesha.
Maagizo hayo ameyatoa katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya kwanza kwa mwaka 2023/2024.
Amesisitiza zaidi kuendelea kuacha maeneo ya wazi yaliotengwa na serikali ili yaweze kusaidia zaidi katika kipindi hiki cha mvua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema tayari Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi Milioni 380 kwa ajili ya kukabiliana na mvua za elnino zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi.
Amesema halmashauri imeona umuhimu wa kutenga fedha hizo kwakuwa tayari tahadhari ilishatolewa dhidi ya mvua kubwa kunyesha.
Hatua za awali ambazo halmashauri zimechukua ni kufanya matengenezo ya barabara ambazo zimeharibiwa na mvua kwa kushirikiana na TARURA.
Kikao cha baraza la Madiwani kimejumuisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali katika ngazi ya kata, halmashauri na Wilaya.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa