Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Maduhu Nindwa ametoa rai kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha kuchukua tahadhari zote za afya ili kujikinga na Magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazotarajia kuanza kunyesha.
Amesema, kipindi hiki cha mvua watu wajitahidi kula vyakula kwa kunawa mikono kwa maji safi na salama na wale chakula cha moto.
Pia, amewataka Mama lishe na Baba lishe waandae chakula katika mazingira safi ili kuwakinga wateja wao wasipate magonjwa ya mlipuko na hata wao wenyewe.
Dkt. Maduhu amesema halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna yakujikinga na magonjwa hayo ya mlipuko.
Vilevile, amezishauri mamlaka za Maji AUWASA na RUWASA kutibu maji na pia wachukue maji katika vyanzo vyenye usalama zaidi.
Akizungumza na Mama lishe na Baba lishe wa soko namba 68 Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa taka na usafi wa mazingira James Lobikoki, amewataka wafanyabiashara wa soko hilo kuzingatia usafi wa mazingira yao ili waweze kuuza vyakula vilivyo safi na salama.
Taarifa ya uwepo wa mvua kubwa ya Elnino iliyotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kuanza mwezi Octoba na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa