Wanawake Jijini Arusha kujengewa uwezo wa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii zao na nchi kwa ujumla.
Kupitia mradi wa " kuongeza ushiriki wanawake kwenye nafasi za uongozi", Shirika la WiLDAF Tanzania limepanga kuhakikisha wanawake na Wasichana wanajiamini katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza katika kikao cha kuutambulisha mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Fatma Amiri ambae ni Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Jiji la Arusha, amesema Jiji la Arusha lipo tayari kushirikiana na wadau hao kwa kuhakikisha wanawake wa Jiji la Arusha wananufaika na mradi huo.
Bi. Fatma amesema, miradi mingi inayoletwa katika Jiji la Arusha imekuwa na manufa sana na mafanikio makubwa hivyo anaamini hata mradi huo mpya utafanikiwa pia.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa WiLDAF Tanzania Bi. Anna Kulaya amesema shirika hilo limejikita zaidi katika katika kuwaboresha wanawake na Wasichana katika nyanja zote.
Nae, mratibu wa Sheria kwa wanawake kutoka shirika la WiLDAF Steven Shishira amesema, mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi kwa Jiji la Arusha utafanyika katika Kata 5 zakuanzia kisha utaendelea kwenye Kata nyingine.
Amesema kinachofanyika katika mradi huo nikubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii kuhusu wanawake kushika nafasi za uongozi lakini pia na wanawake wenyewe kujiamini kuwa wanaweza.
Steve amesema, kupitia mradi huo wanawake watajengewa ari yakuona wanahaki ya kushika nafasi mbalimbali za uongozi na hata wanaume kuwaruhusi wagombe nafasi hizo.
Mradi huu utasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi katika jamii kwani ni nguvu za jinsia mbili zitaweza kufanya kazi kwa pamoja na hivyo kuleta maendeleo katika jamii husika na nchi kwa ujumla.
Mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye fursa mbalimbali za uongozi utafanyika kwa Miaka 3 na maeneo yatayofaidika na mradi huo katika Mkoa wa Arusha ni Halmashauri ya Jiji la Arusha na Halmashauri ya Meru.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa