Jumla ya watoto 104,986 wenye umri wa miaka 5 hadi 14 wa halmashauri ya jiji la Arusha, wamepatiwa dawa za kinga tiba ya ugonjwa wa Kichocho na minyoo ya tumbo. magonjwa yanayofahamika kama magonjwa yasiyopewa kipaumbele 'Neglected Tropical Disease (NTD'.
Zoezi la ugawaji wa dawa hizo lilianza tarehe 2-3/05/2019 katika vituo 154 vilivyoko kwenye shule za msingi za serikali na za binafsi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mganga Mkuu wa halmashauri ya jiji la Arusha, Dkt. Simon chacha amesema kuwa zoezi hilo la kitaifa lilianza na kumalizika salama katika vituo vyote vya kutolea huduma na changamoto ndogondogo zilizojitokeza wakati wa zoezi la utoaji dawa ni baadhi ya wazazi kutotoa ushirikiano wakutosha kwa walimu huku wengi wao kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu kingatiba licha ya kuwa elimu imekuwa ikitolewa mara kwa mara na uongozi wa Halmashauri.
Naye Mratibu wa Kinga Tiba jiji la Bi. Monica Ngonyani, Arusha ameeleza kuwa kutokana na ongezeko la tatizo la magonjwa ya kichocho na minyoo kwa watoto ambayo husababisha upungufu wa damu, utumbo kutoboka na hata kifo, Serikali imeamua kutoa huduma hiyo ya kinga tiba bure nchi nzima.
Ameendelea kwa kusema kua ugonjwa wa kichocho ni tatizo kubwa kwa watoto na usipopata tiba kwa haraka husabisha madhara na wakati mwingine vifo, hivyo ni vema wazazi kuchukua tahadhari kwa kuwapa watoto dawa hizo pindi serikali inapoendesha zoezi la kuwapatia watoto dawa za kinga tiba.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao, wanapata kinga tiba hizo muhimu na kuwaondoa hofu wale wanaodhani dawa hizo zina madhara kwa watoto.
*Pichani: Moja ya wanafunzi wa shule ya Msingi Upendo friends iliyopo kata ya Olmoti Jijini Arusha akimeza dawa wakati wa zoezi la kutoa kinga tiba hizo*
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa