Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Said Mtanda amesema kuwa polio hupelekea ulemavu wa viungo au kushindwa kutembea hivyo ni lazima wazazi na walezi wawapeleke watoto wao kupata chanjo ya polio.
Mtanda aliyasema hayo leo Septemba Mosi, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya ugonjwa wa polio kwa watoto chini ya miaka mitano iliyofanyika kituo cha afya Cha Levolosi.
Alisema chanjo hiyo ni salama na ni njema kwa watoto walio chini ya miaka mitano huku akisisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama na bora kwa afya za watoto.
Alitoa rai kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana na serikali katika zoezi hilo la utoaji chanjo hiyo ya polio na kuongeza kuwa kampeni hiyo ya uchanjaji itavuka lengo ili kila mtoto apate haki yake muhimu ya kiafya.
Alisema serikali inajitajidi kuboresha vituo mbalimbali vya afya ikiwemo maboresho ya huduma za afya kituo cha Levolosi kwani serikali imetoa sh,milioni 500 kwaajili ya kufanya maboresya huduma za afya chakushangaza hela zimekuja lakini hakuna utekelezaji wowote wa maboresho ya huduma za afya.
Alisema inashangaza kuona hela hazijaanza kutumika na wanaambiwa waombe upya, alisisitiza kuwa hatakubali kuona hela zipo lakini utekelezaji wake hakuna.
"Mnaomkwamisha Rais Samia Hassan Suluhu mpo hapa Levolosi na nawaambia tekelezeni majukumu yenu haiwezekani fedha iwepo halafu ikae wee bila kutumika halafu tunaambiwa tuombe tena yani hela imekaa wee bila utekelezaji kwanini nitachukua hatua"
Awali,Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk,Baraka Munde alisema kampeni hiyo ya kitaifa ya Polio inaanza Septemba 1 hadi 4 huku watoto 93,218 wakichanjwa na kupewa dozi hiyo ya polio.
Walengwa kwa siku ni vituo 64 vitatoa chanjo hizo huku dozi 94,000 zikitarajia kutolewa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Aliomba wazazi na walezi kupeleka watoto katika vituo vya afya kwaajili ya kupata chanjo hiyo ya Polio.
Nao baadhi ya wazazi walioshiriki chanjo hiyo ya matone ya polio Lilian Lucas na Julian Samweli waliishukuru serikali kwa kuhakikisha inawakinga watoto hao na ugonjwa huo. Zoezi hilo linafanyika nyumba kwa nyumba ikiwemo vituo mbalimbali vya afya vya Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa