Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid S. Madeni (kushoto) akifanya mahojiano na wafanyakazi wa duka la kuuza na kusambaza dawa za binadamu linalomilikiwa na kampuni ya "Planet Pharmaceutical Limited" juu ya upandishaji bei wa bidhaa aina ya vitakasa mikono "Sanitizer" na barakoa "mask" baada ya ukaguzi wa kushitukiza aliofanya leo Tarehe 21 Machi 2020.
Ukaguzi huu umefanyika katika maduka ambayo yameingia mkataba wa kusambaza dawa vituo vya kutolea huduma za Afya vya Serikali kama mshitiri kujazia zile zinazopatikana Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
kumekuwa na upandishaji bei holela wa bidhaa zinazotumika kujikinga na ugonjwa wa Corona zikiwemo sanitizer na barakoa "mask" tangu ugonjwa huo uliporipotiwa wiki moja iliyopita kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo.
Aidha Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa hizo wala kuzificha vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.Katika ukaguzi huo Mkurugenzi wa Jiji aliambatana na Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Kheri Kagya pamoja na kaimu Mfamasia wa Jiji Ndg. Baraka Ndosi
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa