Katika kuelekea kumaliza mwaka 2017 Msaidizi Afisa Elimu Maalum Bw.Denis Kanana ambaye ndiye mlezi wa shule ya msingi baraa ametoa rai kwa wazazi wa shule hiyo kuonyesha ushirikiano kwa mashirika yanayojitolea kufadhili huduma mbalimbali kwa wanafunzi kwa lengo la kukuza taaluma yao.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na wazazi pamoja na waalimu wa shule ya msingi Baraa katika uwanja wa shule hiyo wakati wa sherehe za kufunga shule .
“ Napenda kutoa pongezi kwa shirika la ITHEMBA kwa kusaidia shule hii kuepukana na adha ya maji ambayo ilikuwa changamoto ya muda mrefu na kuonyesha ushirikiano kwa uongozi wa shule katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi na hatimaye shule ya msingi baraa kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika halmashauri yetu ya jiji la Arusha”. Alisema mlezi huyo
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Ozwin Mosha amewaomba wazazi kuboresha mahusiano mazuri na walimu na kujijengea desturi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuhudhuria vikao vinavyoitishwa na uongozi wa shule kwa mustakabali mzuri wa watoto.
Bi. Fatuma Abdi ambaye ni mratibu wa kata ya Baraa amewataka wazazi kuunga mkono jitihada za serikali juu ya mpango wa elimu bure na kuonyesha mabadiliko kwa mwaka 2018 .
Sherehe ya kufunga shule hufanyika kila mwaka katika viwanja vya shule hiyo ya baraa ambapo kwa mwaka huu wa 2017 imefanyika Tarehe 7/12/2017. shule ya msingi baraa ina jumla ya wanafunzi 1550.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa