Wenyeviti mitaa 10 wapita bila kupingwa
Na Mwandishi wetu
WENYEVITI 10 wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha jana wamekula kiapo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi zilizo wazi uliotakiwa kufanyika Julai Mosi mwaka huu.
Wenyeviti hao baada yakuapishwa na Kamishina wa viapo Wakili Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Jiji la Arusha katika kiapo waliahidi kufanya kazi kwa uadilifu .
Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Arusha Dk.John Pima aliwataka viongozi hao kuheshimu watu wanaowangoza na kuepuka kujiinua kwa sababu Rais Samia Hassan Suluhu hataki viongozi wanaojikweza.
Alisema kitu cha msingi wanatakiwa kufanya kazi lwa ufasaha kwa kutekeleza kazi za wananchi.
"Nyie ni mabalozi wa serikali tushirikiane tufanye kazi kwa pamoja hata mnapokwenda huko maeneo yenu mkazingatie maelekezo yaliotolewa na viongozi wetu wa semta ya afya na mkajiadhari,"alisema.
Aliwasisitiza kuhakikisha wanahimiza wananchi wao kusimamia na kutekeleza maagizo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa kuepuka mikusanyiko, kutumia maji tiririka na kuvaa barakoa.
"Wekeni vitakasa mikono katika ofisi zenu na msiende kuelimisha juu ya hili kwa vitisho na msifukuze watu kwa kutovaa barakoa kwenye ofisi zenu bali waelimisheni, hili ndio jukumu lenu na gonjwa lipo na sisi muingiliano wetu mkubwa na nchi jirani,"alisisitiza.
Dk.Pima alisema walitoa fomu 37 na wenye sifa 27 walionekana na sifa ya kuendelea na uchaguzi wa vyama mbalimbali vya siasa, lakini baadaye mida ulipokaribia walijiondoa katika konyang'anyilo hicho.
Katibu wa Wilaya ya Arusha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Denis Mwita alisema jatima kinyanganyilo hicho walijitokeza wagombea 41 kati yao wanawake sita lakini walioshindwa wanawake wawili na wanaume nane.
Aliwapa pongezi walioshindwa uchaguzi huo kwani kwa chama uchaguzi ni uchaguzi hawana mdogo wala mkubwa,hivyo wao kama chama walijiandaa vema.
"Nendeni mkatunze hadhi ya chama na kuwatumikia wananchi epukeni kujiingiza kwenye ubadhirifu wa kuuza ardhi za wananchi au kujiingiza kwenye migogoro isiyofaa,"alisema.
Pia aliomba Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kutafakari juu ya kuwalipa posho na kuwanunulia vitendea kazi,wenyeviti wa mitaa ili kuwapa moyo wa tendaji kazi humo walipo.
Naye mmoja wa wenyeviti hao Abdallah Mgongo wa Mtaa wa Olmokea alisema atahamasisha wananchi kudumisha amani na utulivu pamoja na kuboresha miundombinu.
Mitaa iliyopata wenyeviti baada ya kupita bila kupingwa ni Mtaa wa Goliondoi Kata ya Sekei,Olmatejo B Kata ya Sakina, Kwamrefu Kata ya Baraa,Kirika B Kata ya Osunyai Jr huku mtaa wa Olkung'u na Erangau kata ya Terrat,Darajani Kata yaUngaltd,Saccon Kata ya Elerai,Block C Kata ya Engutoto na Olmokea Kata ya Sinon.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa