Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Zelothe Steven leo ametekeleza ziara ya kamati ya siasa ya CCM Mkoa na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Arusha leo Tarehe 6/2/2020. katika ziara hiyo alisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe. Joseph Massawe, wajumbe wa CCM secretarieti ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daquarro pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.
Katika ziara hiyo Mhe.Zelothe Steven alitembelea mradi mkubwa wa maji uliopo Ngarramtoni ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu ikiwa dhumuni kubwa la mradi huo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwa maana ya kuongeza mtandao wa kuwasambazia wananchi maji safi.
Akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Gasto Mkawe amesema mradi huo ni sehemu ndogo tu ya mradi mzima kwani mradi wenyewe umegawanyika katika vipengele vitatu ili kurahisisha utekelezaji wake ambapo mradi wote kwa ujumla utagharimu shilingi billion 520 za kitanzania pia amebainisha kuwa uzalishaji wa maji utaongezeka kwa wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.
Mhe. Zolothe Steven amempongeza Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapitia fedha hizo pia amefurahishwa nakasi ya mkandarasi aliyepewa jukumu la kukamilisha mradi huo kwa kasi ya utekelezaji anayofanya.
Mhe. Zolothe Steven pia alitembelea mradi wa barabara ya Ngaramtoni inayoenda paka Usa River barabara ya (By pass) Jijini Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo ya lami yenye urefu wa kilomita 42.4 kutoka Ngaramtoni hadi Usa River ambayo ikikamilika, itapunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Arusha mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 139 fedha za Kitanzania.
Sambamba na hilo Zelothe alitembelea mradi mwingine mkubwa wa maji Jijini Arusha Olasiti (Burka Tenki la maji) ambao ume gharimu shilingi bilioni 2.3 akiwasilisha taarifa ya mradi huo amedokeza kuwa mradi huo utapokea maji kiasi cha lita milioni 3 kutoka katika tenki linguine kubwa lililopo Ngaramtoni.
Naye Mhandisi Gasto Mkawe amesema wanufaika wa mradi husika ni wakazi wa Kata za Olasiti, Sombetini, Osunyai, Sokoni 1, Murieti, na Terrati wapatao 156,320 nakuongeza kuwa pamoja na tenki hili kujengwa pia AUWSA imepanga kujenga matenki mengine 11 katika maeneo mengine likiwemo lile la Ngorbob, Olmoti, Mlima ccm,Themi, Moshono, Moivo na mengineyo.
Ziara hiyo iliendelea hadi kituo cha Afya Murieti mbapo Mhe Zolothe alipokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Simon Chacha.
Dkt. Chacha amesema kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho ume gharimu jumla ya shilingi bilioni moja milioni miamoja sabini na tisa mianne arobaini kati ya fedha hizo fedha, milioni mianne sabini na tisa mianne arobaini zimetolewa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa maana ya makusanyanyo ya ndani na Serikali kuu ilitoa jumla ya shilingi milioni miasaba . pia ameishukuru serekali ya Jamuhuri ya muungano chini ya Mhe. Dkt. Joh Pombe Magufuli kwakutoa fedha zilizo saidia kukamilika kwa mradi huo.
DktChacha alidokeza kuwa kituo hicho kimeanza kutoa huduma za kumuona Daktari, maabara, kulaza wagonjwa kwa mda pia huduma za VVU na UKIMWI , huduma za mama na mtoto pamoja na upasuaji mdogo na kusema kuwa kabla ya mwezi huu kuisha kituo hicho kitaanza kutoa huduma za upasuaji kwa kina mama
Dkt. Chacha alisema kuwa lengo kubwa ni kusaidia kata ya murieti yenye Wananchi wapatao 56,000 alieleza kuwa kata hiyo ina mitaa 13 lakini kata yote haikuwa na kituo cha afya. Baadaye Mhe. Zelothe alitembelea Shule ya Sekondari ya Arusha Terrat, mradi wa maji machafu uliopo Terrat ambao upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake, Hospitali ya Wilaya ya Engutoto na kituo cha afya Moshono.
Mhe. Zelothe Steven amefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo alisema pia ilani inayo tekelezwa ni ilani ya CCM inayo elekeza kuwa kila Kata iwe na kituo cha afya na uboreshaji wa miundo mbinu kwa hali ya juu. “Kwahiyo Serikali ya CCM ni dhahiri kusema kwamba inatekeleza kile walicho ahidi kwa wananchi wake nakuwaahidi kwamba hayo ni matokeo ya awali yapo matokeo mazuri yanafuata” alisema Zeloth.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa