Na Mwandishi Wetu
Arusha
Mkoa wa Arusha umepata fedha Kiasi cha shilingi Bilioni 1. 372 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa, ujenzi wa vyoo na mabweni 4 katika Shule ya sekondari Arusha girls iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na Shule ya Sekondari ya Florian iliyopo Wilayani karatu.
Akizungumza katika hafla ya Kusainisha mikataba ya kusimamia ujenzi huo iliyofanyika mapema leo Aprili 29,2023, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela Amesema mkoa wameamua kusainishana mikataba ya ujenzi huo na wahusika wakuu ambao ni mkuu wa wilaya ya karatu , Mkurugenzi wa Jiji la Arusha na wakuu wa shule hizo.
Mhe. Mongella amesema kazi za ujenzi wa shule hizo zinatakiwa kukamilika ndani ya siku 90 na vigezo vyote vinavyohitajika kwenye ubora wa majengo vimeainishwa kwenye mkataba huo .
"Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anaendelea kuleta fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta ya hii nyeti ya elimu na mnajua kwenye mkoa wetu tulishapokea Awali Bilioni 6.8 Mpango wa Boost Sasa tumepata kwenye sekondari hizi mbili kwa msimu huu " alisema Mongella.
Pia amewataka wakuu wa shule hizo kutumia vizuri fedha walizopatiwa na kufuata maelekezo yaliyotolewa ya Ujenzi wa shule zenye viwango bora na ujenzi wa uhakika kwakuwa fedha walizopatiwa zinatosheleza mahitaji ya ujenzi hadi kukamilika.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hargney Chitukuro amesema wapokea Kiasi Cha fedha shilingi milioni 679.1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15, mabweni 2 na matundu ya vyoo 21 kwenye Shule ya Arusha Girls sekondari.
"Nitakwenda kusimamia kwa kushirikiana na wenzangu kuhakikisha kwamba fedha Hizi zinakamilisha ujenzi wa miundombinu hii niliyoisema Kama ambavyo imepangwa nasio vinginevyo na tutaikamilisha kwa ubora na Kwa wakati "amesema Chitukuro.
Aidha Chitukuro ameishukuru Serikali kwa kiasi hicho cha fedha walichokipata kwakua msimu watakao ripoti wanafunzi wa kidato cha tano mwezi Julai mwaka huu watakuta miundombinu bora Shuleni.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Arusha Mwl. Abeli Ntupwa ameeleza kuwa fedha hizo zimelenga kuandaa mazingira bora ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano ambao wanatarajiwa kuripoti Shule kwanzia mwezi Julai mwaka huu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa