Halmashauri ya Jiji la Arusha inatarajia kutoa zaidi ya Tsh. milioni 270 kwa ajili ya vikundi vya kina mama, vijana na walemavu katika robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Ndg. Grayson Orcado ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ghafla ya mafunzo ya ujasiriamali kwa walengwa wa mikopo yaliyofanyika hapo jana katika ukumbi wa shule ya msingi Arusha.
AIdha Kaimu Mkurugenzi alitoa rai kwa Walengwa hao wa mikopo kuwa fedha wanazopatiwa sio msaada bali zinatakiwa kurejeshwa kwa wakati na kuzifanyia shughuli zilizokusudiwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo binanfsi na Taifa kwa ujumla.
“Mafunzo haya yanalenga kuwawezesha wanawake, watu wenye ulemavu na vijana na jamii kwa ujumla kuweza kujiajiri. kuwafanya wanawake na vijana watambue wajibu wao katika kujiletea maendeleo na kuifanya jamii kutambua fursa mbalimbali zilizo za halali katika maeneo yanayowazunguka.” Alisema Ndg. Orcado.
Naye Kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Tajieli Mahega amevipongeza vikundi vilivyopita katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kurejesha fedha kwa wakati hali iliyochaingia kufanikisha zoezi la utolewaji wa mikopo kwa mwaka huu mpya wa fedha tulionao.
“vikundi vimeweza kujipatia maendelo ya wao wenyewe kwa kufanya biashara ndogondogo na hivyo wameweza kujikimu katika malazi, chakula na mavazi. wanawake, walemavu na vijana wa jiji la Arusha wanaheshimika kwa kuwa sasa wanao uwezo wa kufanya biashara na kupata fedha za kujikimu” alisema Bi. Tajiel wakati akisoma taarifa yake kwa mgeni rasmi.
Jumla ya vikundi vinavyotarajia kupata mkopo huo ni 55 ambapo vya wanawake ni 34 na vijana ni 21.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa