Kamati ya Siasa ya halmashauri kuu wilaya ya Arusha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Bwana Joseph Masawe wametembelea miradi ambayo imetekelezwa na ilani ya chama hicho kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Tarehe 1 Octoba 2019.
Kamati hiyo imetembelea miradi 10 ikiwemo Tenki la maji ESAMI, Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi hospitali ya wilaya, Matundu ya vyoo 20 shule ya msingi Murriet Darajani, Matundu ya vyoo 10 shule ya msingi sokoni I, Ujenzi wa Daraja la Shaulalu kata ya Sokon 1, ujenzi wa madarasa 4 ya ghorofa shule ya Sekondari Sombetini,ujenzi wa uzio katika kituo cha afya daraja II,ujenzi wa barabara ya Masjid Quba na barabara ya Sanawari pamoja na Vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo kata ya Ngarenaro.
Akizungumzia miradi hiyo iliyotembelewa Mwenyekiti Masawe amesema kuwa ziara hiyo ni ya kawaida na ikiwa na lengo la kuhakikisha yale ambayo yaliahidiwa chini ya ilani ya Chama cha mapinduzi kupitia Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanatekelezwa kwa wakati.
Aidha amesema chama cha mapinduzi kiko makini katika kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa pamoja na yale waliyoahidi kupitia serikali ya awamu ya tano yanatekelezwa ikiwemo suala la Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara pamoja na maji.
Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa matundu 30 ya vyoo katika shule mbili za msingi Murriet na Sokon 1 ambayo yako katika hatua za umaliziaji huku akitoa maagizo kwa mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa madarasa 4 ya Ghorofa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini kukamilisha ujenzi huo unakamilika mapema ndani ya muda wanyongeza aliopewa kwani ameonekana akichelewesha ujenzi kinyume na mkataba unavyoelekeza.
Pia kamati hiyo ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kimewapongeza watendaji wa serikali ambao wamekuwa makini kusimamia miradi ya maendeleo hasa katika kuelekea katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa. Joseph Massawe amesisitiza pia ushirikiano baina ya watumishi na wakandarasi ili kupelekea miradi inapoanzishwa itekelezwe kwa wakati na kuepusha vikwazo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa