TAARIFA YA KATA YA SEKEI.
UTANGULIZI
Kata ya Sekei ni miongoni mwa kata 25 za Halmashauri ya jiji la Arusha. Kata hii inapakana na kata ya kimandolu upande wa magharibi, kaloleni upande wa mashariri, kusini kata ya Oloirieni na kaskazini inapakana na Halmashuri ya Arusha. Kata ya sekei ina jumla ya mitaa sita ambayo ni: Naura, AICC, Goliondoi, Mahakama, Sanawari, Naurei.
HISTORIA YA KATA.
Kabla ya kuwa kata ilikua tawi ambalo lilikuwa likuhudumiwa na makatibu wa CCM.Kata ya sekei ilianzishwa mnamo mwaka 1969. Jina sekei limetokana na neno la kimasai seki. Seki ni aina ya miti iliyokuwa imeota katika maeneo ya kata na ilikua ni malisho mazuri ya mbuzi.
Asili ya watu wa sekei ni mchanganyiko wa wamasai, wameru,na wachaga waliotokea kijiji kinachoitwa Mula.
Kata ina jumla ya wakazi 9213 ME 4272 na KE 4941.
IDADI YA SHULE
Kata ina jumla ya shule tatu za msingi ambazo ni Kijenge, Sanawari na Naura na kila shule ya msingi ina madarasa ya awali. Kata haina shule ya sekondari.
VITUO VYA AFYA.
Kata ina kituo cha afya cha Polisi Pamoja na hospitali ya mkoa Mount Meru.
TAASISI ZA SERIKALI.
Taasisi za serikali zilizopo kata ya sekei ni kama ifuatavyo;
MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Kwa mwaka huu wa fedha. Miradi inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Matundu ya vyoo shule ya msingi sanawari na kijenge, ukarabati wa soko la sanawari, taa za barabarani,marekebisho ya barabara zinazoingia ndani ya kata
MIPANGO YA KATA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANACHI.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa