WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAAPISHWA
Posted on: November 21st, 2019Jumla ya wasimamizi 30 wa Vituo vya kupiga kura wameapishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema leo Tarehe 21 Novemba 2019 na Hakimu Mkazi Mhe. Itikija Theoflo Nguvava .
Akizungumza na wasimamizi hao baada ya kuapishwa Ndg.Msena Bina ambae ni msimamizi wa uchanguzi Wilaya ya Arusha amesema ni muhimu wasimamizi kuzingatia kiapo hicho cha utii, uadilifu na uaminifu kwani ndicho kitakacho waongoza katika kuwasimamia wapigakura ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wapiga kura ni Raia wa Tanzania, asiye na umri chini ya miaka 18, Mkazi wa Mtaa husika, aliye jiandikisha katika daftari la wapiga kura na awe anaakili timamu.
Hata hivyo Ndg.Msena amesema mpiga kura awe na kitambulisho chochote kitakacho mtambulisha chenye picha yake mfano kitambulisho cha Utaifa, cha mpiga kura, Bima ya afya, Leseni ya udereva na Pasi ya kusafiria .
Pamoja na hayo wasimamizi wamehimizwa kuzingati muda wa kufungua na kufunga vituo ambapo ni saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 10:00 Jioni na kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu, wazee, wamama wajawazito na wanaonyonyesha.
“Tume waamini ndio maana tumewateua hivyo mzingatie viapo vyenu mkafanye kazi kwa uadilifu, uaminifu na utii pia katika kipindi hiki epukeni kutumia vilevi” alisema Ndg.Msena Bina.
Mwisho.