• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 43 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI "MSIMAMO WETU NI KUTEKELEZA YALE TULIYO AHIDI UCHAGUZI MKUU".

Posted on: February 6th, 2020

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  Mhe. Zelothe Steven leo ametekeleza ziara ya kamati ya siasa ya CCM Mkoa na kutembelea miradi  mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Arusha leo Tarehe 6/2/2020. katika ziara hiyo alisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe. Joseph Massawe, wajumbe wa CCM secretarieti ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daquarro pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.

Katika ziara hiyo Mhe.Zelothe Steven alitembelea mradi mkubwa wa maji uliopo  Ngarramtoni ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu ikiwa dhumuni kubwa la mradi huo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa maji  kwa maana ya kuongeza mtandao wa kuwasambazia wananchi maji safi.

Akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA  Mhandisi Gasto Mkawe amesema mradi huo ni sehemu ndogo tu  ya mradi mzima kwani mradi wenyewe umegawanyika katika vipengele vitatu ili kurahisisha utekelezaji  wake  ambapo mradi wote kwa ujumla  utagharimu shilingi billion 520 za kitanzania pia amebainisha kuwa uzalishaji wa maji utaongezeka kwa wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.

Mhe. Zolothe Steven amempongeza Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapitia fedha hizo pia amefurahishwa nakasi ya mkandarasi aliyepewa jukumu la kukamilisha mradi huo kwa kasi ya utekelezaji anayofanya.

Mhe. Zolothe Steven pia alitembelea mradi wa barabara ya Ngaramtoni  inayoenda paka Usa River barabara ya (By pass) Jijini Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo ya lami yenye urefu wa kilomita 42.4 kutoka Ngaramtoni hadi Usa River ambayo ikikamilika,  itapunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Arusha mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 139 fedha za Kitanzania.

Sambamba na hilo Zelothe alitembelea mradi  mwingine mkubwa wa maji Jijini Arusha Olasiti (Burka Tenki la maji) ambao ume gharimu shilingi bilioni 2.3 akiwasilisha taarifa ya mradi huo amedokeza kuwa mradi huo utapokea maji kiasi cha lita milioni 3 kutoka katika tenki linguine kubwa lililopo Ngaramtoni.

Naye Mhandisi Gasto Mkawe  amesema wanufaika wa mradi husika ni wakazi wa Kata za Olasiti, Sombetini, Osunyai, Sokoni 1, Murieti, na Terrati wapatao 156,320 nakuongeza kuwa pamoja na tenki hili kujengwa pia AUWSA imepanga kujenga matenki mengine 11 katika maeneo mengine likiwemo lile la Ngorbob, Olmoti, Mlima ccm,Themi, Moshono, Moivo na mengineyo.

Ziara hiyo iliendelea hadi kituo cha Afya Murieti  mbapo Mhe Zolothe alipokea taarifa ya utekelezaji  kutoka kwa Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Simon Chacha.

Dkt. Chacha amesema  kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho ume gharimu jumla ya  shilingi  bilioni moja  milioni miamoja sabini na tisa mianne arobaini kati ya fedha hizo fedha, milioni mianne sabini na tisa mianne arobaini zimetolewa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa maana ya makusanyanyo ya ndani na Serikali kuu ilitoa  jumla ya shilingi milioni miasaba . pia ameishukuru serekali ya Jamuhuri ya muungano chini ya Mhe. Dkt. Joh Pombe Magufuli kwakutoa  fedha zilizo saidia kukamilika kwa mradi huo.

DktChacha alidokeza kuwa kituo hicho kimeanza kutoa huduma za kumuona Daktari, maabara, kulaza wagonjwa kwa mda pia huduma za VVU na UKIMWI , huduma za mama na mtoto pamoja na upasuaji mdogo na kusema kuwa kabla ya mwezi huu  kuisha kituo hicho kitaanza kutoa huduma za upasuaji kwa kina mama

Dkt. Chacha alisema kuwa lengo kubwa ni kusaidia kata ya murieti yenye Wananchi wapatao 56,000 alieleza kuwa kata hiyo ina mitaa 13 lakini kata yote haikuwa na kituo cha afya. Baadaye Mhe. Zelothe alitembelea Shule ya Sekondari ya Arusha Terrat, mradi wa maji machafu uliopo Terrat ambao upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake, Hospitali ya Wilaya ya Engutoto na kituo cha afya Moshono.

Mhe. Zelothe Steven amefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo  alisema pia ilani inayo tekelezwa  ni  ilani ya CCM inayo elekeza kuwa kila Kata iwe na kituo cha afya na uboreshaji wa miundo mbinu kwa hali ya juu. “Kwahiyo  Serikali ya CCM ni dhahiri kusema kwamba inatekeleza kile walicho ahidi kwa wananchi wake nakuwaahidi kwamba hayo ni matokeo ya awali yapo matokeo mazuri  yanafuata” alisema Zeloth.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI June 19, 2025
  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa