Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amekabidhi hundi ya shilingi 626,866,000 kwa vikundi 100 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni fedha zinazotokana na sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Daqarro amekabidhi hundi hiyo leo Tarehe 09 Juni 2020 na kuvitaka vikundi vilivyo nufaika na mkopo huo kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyo kusudiwa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi, pamoja na kurejesha fedha hizo kwa wakati ulio pangwa ili vikundi vingine viweze kunufaika.
Amesema vikundi 109 viliomba mikopo hiyo lakini vikundi 9 kati ya hivyo havijapata mkopo kwasababu wamekosa sifa nakuitaka idara ya maendeleo ya Jamii ambayo inayoshughulikia mikopo hiyo kusaidia vikundi hivyo kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili waweze kupata mkopo kama vikundi vingine.
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni amevieleza vikundi kuwa Halmashauri inatazamia kuboresha mikopo hiyo kwa maana ya kuongeza kiwango cha mikopo pamoja na kununua vitendea kazi kama vile mashine za kusaga nafaka, mashine za kushona nguo na mashine za kufyatua matofali. Maboresho haya alisema kuwa yataweza kukidhi mahitaji ya vikundi pamoja na kuongeza uzalishaji kwa pato la taifa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa