1.0.UTANGULIZI
Mipango miji ni Idara muhimu katika Jiji la Arusha inayosimamia mpangilio wa Mji na matumizi bora ya Ardhi. Kazi zinazofanyika katika Idara hii ni
i.Kuanda michoro ya mipango miji kwenye maeneo yaliyoiva , kuendelezwa kwa kushirikisha wananchi wa maeneo husika.
ii.Kuandaa michoro ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela kwa kushirikisha wananchi wa maeneo husika.
iii.Kuandaa michoro ya marekebisho ya mipangomiji katika maeneo ambayo michoro iliandaliwa lakini imepitwa na wakati.
iv.Kutoa masharti ya uendelezaji wa Ardhi katika viwanja mbalimbali.
v.Kuchambua, kukagua na kuandaa mapendekezo ya mabadiliko ya matumizi ya Ardhi na umedgaji wa viwanja na kuwasilisha kwenye ngazi zinazohusika.
vi.Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mipangomiji katika uendelezaji wa ardhi
vii.Kupitia na kupitisha maombi ya vibali vya ujenzi.
viii.Kushiriki katika kuandaa mpango kabambe wa Jiji.
1.1.UTARATIBU WA KUPATA HATI
Mwananchi /mmiliki aleta wa ardhi ili aweze kupata Hati anatakiwa kuwasilisha vitu vifuatavyo kwa Afisa Ardhi
i.Picha tano pastport size.
ii.Mhutasri wa Kata
iii.Kitambulisho chake
iv. Ramani ya upimaji wa eneo / kiwanja husika .
Baada ya kuwasilisha vitu tajwa hapo juu Mwanachi/mmiliki atatakiwa
i.Ajaze form ya maombi Na.19 na kusaini
ii.Mwanachi kuonyesha kiwanja chake.
Kisha wataalam wa Ardhi watafanya kazi zifuatazo:
i.Faili ifunguliwe na ipelekwe mipangomiji kw ajili ya masharti/matumizi.
ii. Kuandaa form ya malipo/ advice of payments.
iii.Malipo stahiki kwa ajili ya maandalizi ya hati.
iv.Mmiliki anasaini fomu ya kukiri malipo/ acknowledgement for payments.
v.Deed plan zinachorwa kuandaa mchoro wa ramani ndogo ya kiwanja husika.
vi.Rasimu ya hati huchapwa pamoja na majalada ya hati
vii.Mwananchi anasaini hati yake na Historia ya kiwanja inaadnaliwa na rasimu za hati pamoja na vitambulisho muhimu kupelekwa kwa kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya moshi.
viii.Rasimu zikishafika kwa kamishina msaidizi wa ardhi ,zinakaguliwa na endapo atajiridhisha, atazipitisha kwa kutia sahihi yake.
ix.Hati ikishasainiwa na kamishna msaidizi wa Ardhi hupelekwa kwa msajili wa hati kwa ajili ya usajili.Kwa msajili ada ya usajili lazima ilipwe ndipo hati iweze kusajiliwa.
NB:Hati ikishasajiliwa kwa msajili na mmliki hupewa hati yake na kukabidhiwa fomu ya usajili huletwa ofisi ya ardhi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu. Upatikanaji wa Hati huchukua muda wa miezi mitatu.
1.2.LIPA KODI YA ARDHI KILA MWAKA – NI MKATABA KATI YAKO NA SERIKALI.
Mmiliki wa ardhi anapaswa kulipa kodi ya pango la ardhi kila ifikapo tarehe 1 Julai ya kila mwaka. Kodi ya ardhi ikichelewa kulipwa kwa miezi sita ,itatakiwa kulipwa pamoja na adhabu. Kodi ikilazwa itatakiwa kulipwa pamoja na adhabu na malimbikizo kwa mujibu wa sheria.
Wamiliki wa ardhi ni wapangaji ambao Uhalali wao unatokana na kulipa kodi ya pango na kutokulipa kodi ya pango la Ardhi kwa wakati ni kuvunja mashati ya kumiliki ardhi.
HASARA ZA KUTO KULIPA KODI YA ARDHI:-
Wamiliki wa ardhi wanapata fursa ya kutumia ardhi ya umma badala ya wananchi wengine .
•Hivyo wasipolipa kodi ,wanawadhulumu wale waliokosa fursa ya kuitumia ardhi hiyo.
•Wanachochea ujenzi holela, wanaiibia serikali na kukwamisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
FAIDA ZA KULIPA KODI YA ARDHI:-
•Kodi ya ardhi ,huchangia Miji na makazi kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na viwanja kwa ajili ya ujenzi.
•Mapato ya kodi , huiwezesha serikali kuchangia kupanga miji, kuendeleza upimaji na utoaji wa viwanja kwa wananchi kwa matumizi mbalimbali.
GHARAMA ZA KUCHELEWA KULIPA KODI KWA WAKATI:-
•Serikali imetoa notisi ya siku 90 kuanzia 1 machi,2005, kwa watu wote wanaomiliki ardhi wenye madeni ya pango la ardhi kulipa madeni hayo mara moja .
• Baada ya muda huo, serikali itachukulia kuwa wadaiwa hawa wanavunja kwa makusudi sharti hili la kumiliki ardhi.Serikali itatekeleza sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, kwa kuchukua hatua ya kufuta haki zao za miliki ardhi na kuwafungulia kesi mahakamani madeni ya kodi ya ardhi.
•Ardhi hiyo na maendelezo yake vitanadiwa na kumilikishwa kwa watu wengine ,na mmilikaji aliyefutiwa miliki atalipwa fidia ya maendelezo yake katika ardhi, baada ya kukata deni la kodi ya pango la ardhi.
FAIDA ZA UMILIKI HALALI WA ARDHI:-
•MIliki halali ya ardhi yenye hati iliyo sajiliwa n akulipiwa kodi ya Ardhi ni fursa tosha ya kujipatia mitaji ya maendeleo.
•Mmiliki wa ardhi mwenye upeo wa maendeleo huhalalisha miliki yake kwa kulipia kodi ya pango la ardhi na kutumia umiliki wake wa ardhi kujiletea maendeleo,yeye na familia yake na jamii nzima kwa ujumla.
NB: MMILIKI WA ARDHI, LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KIJIEPUSHA NA MATATIZO YA KUNYANG’ANYWA ARDHI NA KUFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa