TAARIFA YA KATA YA ELERAI
UTANGULIZI:
Kata ya Elerai ni miongoni mwa kata 25 zinazounda Jiji la Arusha. Kata hii ina kaya 6052 na wakazi wa kata hii ni 28,813.
UTAWALA:
Kata hii ina watumishi 13 nao ni;
Afisa Afya
Afisa maendeleo ya jamii
Mratibu wa Elimu
Afisa mifugo
Watendaji wa mitaa 6
Walinzi 2
Afisa mtendaji wa kata.
ULINZI NA USALAMA.
Hali ya ulinzi na usalama ni nzuri kwa kipindi chote cha miezi mitatu (3) hakuna tukio lolote la uhalifu lililotokea katika kata. Ulinzi unaotumika katika kata ni wananchi kujilinda wenyewe kwa kuweka zamu.
KUITISHA VIKAO VYA MITAA:
Kwa kipindi cha mwezi May – Julai vimefanyika vikao 39 na kukamilisha muhtasari 39.
MAENDELEO YA KATA YA ELERAI.
Kata ya Elerai inatoa pongezi kubwa kwa maendeleo ya Kata yaliyofanyika hususani kama ifuatavyo:
Ujenzi wa paa la pili la soko lenye thamani ya Tsh.100,000,000/=
Ujenzi wa Zahanati umekamilika
Ujenzi wa madarasa manne ya Sekondari ya Elerai yenye
Ukarabati wa madarasa matatu ya shule ya sekondari elerai yenye thamani ya Tsh.1,3000,000/=
USAFI WA MAZINGIRA:
Hali ya usafi wa mazingira inaridhisha kwani wananchi wamehamasika kufanya usafi wa maeneo yao yote yanayowazunguka.
Elimu ya usafi inaendelea kuimarika kulingana na siku tunazofanya usafi ya Jumamosi ya kwanza ya mwezi na ya mwisho wa mwezi kila mwezi.
USAFI WA SOKO LA ELERAI:
Kwa ushirikiano wa watendaji wa mitaa pamoja na wafanyabiashara wa soko tunafanya usafi ndani na nje ya soko pamoja na vyoo vya soko.
USAFI WA BARABARA YA MAJENGO NA MITARO
Usafi huu ulifanyika vizuri kushirikiana na wafanyabiashara walioko maeneo hayo kando kando ya bara bara na ndani ya mitaro.
UKAGUZI WA MAZINGIRA WA MAMA LISHE.
Wafanyabiashara wa mama lishe wamekaguliwa na kupewa elimu kuhusu kuvaa uniform (sare za kazi) wanapokuwa kwenye biashara zao, maji ya wateja ya kunawia mikono yawe moto kulipia shilingi elfu tano (5000) na kupima afya zao, kusafisha maeneo wanayofanyia biashara na kuahakikisha yawe masafi siku zote.
TAARIFA YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
0.1 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA.
1.1 KUFUATILIA MAREJESHO YA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE.
Kwa kata ya Elerai vikundi viatatu (3) vya wadaiwa sugu, kikundi kimoja kipo mtaa wa Samanga kinaitwa Maisha Plus na viwili majengo A ambavyo ni Tukundane na Tarajio W. Group. Ufuatao ni mchanganuo katika Jedwali.
JINA LA KIKUNDI |
MWAKA |
MKOPO |
MKOPO + RIBA |
REJESHO |
SALIO |
TARAJIO W. GROUP
|
2014
|
2,000,000/=
|
2,200,000/=
|
1,824,000/=
|
376,000/=
|
TUKUNDANE
|
2014
|
1,500,000/=
|
1,165,000/=
|
1,030,000/=
|
620,000/=
|
MAISHA PLUS
|
2010
|
1,000,000/=
|
1,100,000/=
|
550,000/=
|
550,000/=
|
JUMLA
|
|
4,500,000/=
|
4,950,000/=
|
3,404,000/=
|
1,546,000/=
|
Kwa Kata ya Elerai kikundi cha Vijana wadaiwa sugu ni kimoja tu. Kipo Mtaa wa Remtula.
JINA LA KIKUNDI |
MWAKA |
MKOPO |
MKOPO + RIBA |
REJESHO |
SALIO |
GLOFAHABEEL
|
2014
|
1,500,000/=
|
1,650,000/=
|
1,462,500/=
|
187,500/=
|
JUMLA
|
|
1,500,000/=
|
1,650,000/=
|
1,462,500/=
|
187,500/=
|
1.2 USIMAMIZI UJAZAJI WA MIKATABA
Niliweza kusimamia ujazaji Mkataba kikoba cha UMJ kilichopitishwa na WDC kitakachotumika kupitishia Mikopo ya vikundi vingine, pia niliwakutanisha na viongozi wa vikundi vilivyoomba mkopo mwaka 2016 kwa majina ni B. Mabaju, Sindeni, Usia na Neema Limca.
KUKUTANA NA VIKUNDI NA KUTOA USHAURI/ MAELEKEZO.
Kukutana na vikundi na kutoa ushauri kuhusu usajili wa vikundi, pia kutoa ushauri mambo ya kiuchumi kama vile kila Mwanakikundi awe na shughuli ya kumpatia kipato. Na wote kwa pamoja wawe na malengo ili wanaposema wanavunja mzunguko wapeane mrejesho walichofanikiwa na sio kukiri kwa kugawana faida tu.
NA. |
JINA LA KIKOBA |
MTAA KILIPO |
|
HAPA KAZI TU
|
SHAMSI
|
|
NIWEZESHE
|
SHAMSI
|
|
FUTURE
|
MAJENGO B
|
|
WAWAEL
|
MAJENGO B
|
|
ALFA
|
MAJENGO A
|
|
UKOMBOZI
|
BURKA
|
1.4. KUSIMAMIA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASKINI.
Mpango huu unaendeshwa na TASAF awamu ya tatu, nimekuwa nikishiriki awamu zote mbili kwa malipo ya miezi miwili miwili, kwa awamu zote mbili huwa nashiriki katika mitaa 04 kwa muda wa siku nne. Tarehe 23 – 26/5/2016 nishiriki mitaa ifuatayo RC kata ya Mushono, Jamhuri kata ya daraja mbili, Olmatejo B kata ya Sakina, Majengo kata ya Levolosi. Tarehe 1/8/2016 – 4/8/206 nilishiriki Mitaa ya mita 200 Ngarenaro, Daraja mbili, Sokoni 1 na Olorieni.
1.5: KUANDAA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
Kusimamia maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika tarehe 16/6/2016 shule ya msingi Burka. Walitoa ujumbe kuhusu haki za watoto kwa njia ya nyimbo, shairi, ngonjera. Watoto walitoa msisitizo kwa jamii kushiriki kuwalinda na vitendo vya kikatili.
1.6: KUWASILISHA/ KUHAKIKI MAJINA KAMILI YA WATOTO WALIOOMBA KUPEWA MAHITAJI YA SHULE.
Majina kumi (10) tu ndio walioomba kupatiwa mahitaji ya shule na ndio yalipitishwa na WDC na kuwasilisha majina hayo ofisi ya maendeleo ya jamii depot.
1.7: UCHAGUZI WA KAMATI YA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI YA KATA.
Kamati hii ilichaguliwa kwa kufuata muundo, walipatiwa mafunzo tarehe 15/7/2016 shule ya msingi Meru, ili kushirikiana na kamati za mitaa kutoa huduma kwa watoto hao.
1.8: UCHAGUZI KUHUSU TIBA KWA KADI (TIKA)
Elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kwenye mikutano ya mitaa na vikundi vya jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na tika.
2. MIKOPO
Vikundi vya wadaiwa sugu wamepewa ilani ya miezi mitatu (3) wawe wamemaliza kurejesha mkopo wa kikundi. Wenyeviti wa mitaa vikundi vilipo wamepewa nakala ya ilani kwa usimamizi na Mh. Diwani kwa ufuatiliaji, hivyo nahitaji ushirikiano
Wanakikundi ambao hawajulikani walipohamia tushirikiane na wenyeviti wa mitaa husika na wanakikundi waliobaki ili kujua walipohamia.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI – IDARA YA ELIMU TAREHE 9.8.2016.
UTANGULIZI:
Shule zilizopo katika kata ambazo zina usajili ni kama ifuatavyo:
SERIKALI:
Elerai msingi, Azimio s/msingi, Burka s/msingi na Elerai sekondari.
BINAFSI:
Arusha Modern, Arusha Intergrated, Majengo, St. Thadeus, Joseph zote hizi ni za msingi na Sekondari ya Bishop Kisula.
IDADI:
Shule za serikali zina idadi ya wanafunzi na madawati kama ifuatavyo:
JINA LA SHULE |
IDADI YA WANAFUNZI |
MADAWATI |
||||
WAV
|
WAS
|
JML
|
HITAJIKA
|
YALIYOPO
|
PUNGUFU
|
|
BURKA
|
580 |
607 |
1187 |
392 |
423 |
- |
AZIMIO
|
393 |
413 |
806 |
280 |
289 |
- |
ELERAI S/MSINGI
|
862 |
884 |
1746 |
581 |
591 |
- |
ELERAI SEK
|
643 |
710 |
1353 |
1353 |
1353 |
- |
MIUNDO MBINU:
JINA LA SHULE |
MATUNDU YA VYOO |
VYUMBA VYA MADARASA |
||||
HITAJIKA
|
ILIYOPO
|
PUNGUFU
|
HITAJIKA
|
VILIVYOPO
|
PUNGUFU
|
|
BURKA
|
WAV: 23
53 WAS: 3O |
24
|
29
|
27 |
23 |
4 |
AZIMIO
|
WAV: 16
37 WAS: 21 |
10
|
27
|
19 |
11 |
8 |
ELERAI S/MSINGI
|
WAV: 34
78 WAS: 44 |
8
|
70
|
39 |
17 |
22 |
ELERAI SEK
|
WAV: 25
60 WAS: 35 |
20
|
40
|
30 |
23 |
7 |
|
UWIANO: MATUNDU YA VYOO
|
VYUMBA VYA MADARASA |
||||
|
WAV: 1: 25
WAS: 1: 20 |
1: 45 |
MAFANIKIO:
Shule zote zina madawati ya kutosh na hakuna upungufu.
Kukamilika kwa vyumba vinne vya madarasa Elerai Sekondari, pamoja ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa.
Kukarabatiwa kwa vyoo matundu 8 shule ya msingi Elerai na viko katika hali nzuri.
Mfadhili AVCO ameanza kujenga vyumba viwili S/M Elerai vipo hatua ya msingi. Pia kufunika shimo kubwa la choo.
Hali ya taaluma mashuleni ni nzuri. Hii ni kutokana na matokeo ya majaribio mbali mbali yanayofanyika.
Fedha za elimu msingi zimeendelea kutumwa shuleni, kutoka Januari – Machi zimepokelewa kama ifuatavyo:-
ELERAI |
BURKA |
AZIMIO |
ELERAI SEKONDARI |
5,555,000/=
|
4,261,000/=
|
3,461,000/=
|
Fidia ya ada: 16,261,000/=
Capitation: 15,364,000 |
CHANGAMOTO:
Mapungufu ya matundu ya vyoo kama ilivyo kwenye jedwali. Ni pamoja na vyumba vya madarasa na miundo mbinu ya kupekeka maji kwenye vyoo vinavyotumiwa na wavulana Elerai Sekondari.
Tatizo la nyumba za walimu Shule ya msingi Burka zilizopo ndani ya eneo la Elerai sekondari.
Nyumba ya Mwl. iliyopo Elerai Sekondari ambayo inahitaji kukamilishwa.
Kukosekana kwa uzio wa shule kwa shule zote za msingi.
Kutokuwepo kwa majengo ya utawala kwa shule ya Azimio, Elerai s/msingi, Elerai Sekondari na kusababisha kubadili chumba cha darasa kuwa ofisi.
Kukosekana kwa stoo hasa kwa shule ya Elerai s/msingi na Azimio s/msingi.
Baadhi ya wazazi kutokuona umuhimu wa uchangiaji chakula shuleni japo elimu inaendelea kutolewa.
MIFUGO:
IDADI YA MIFUGO NA KAYA:
KAYA ZINAZOFUGA
|
NG’OMBE
|
MBUZI
|
KONDOO
|
MBWA WAFUGWAO
|
KUKU
|
BATA
|
74
|
185
|
105
|
25
|
10
|
1162
|
78
|
LISHE KWA MIFUGO:
Hali ya malisho na maji ni ya kuridhisha.
MIUNDO MBINU YA MIFUGO
Hakuna miundo ya mifugo
MAGONJWA
Magonjwa yaliyojitokeza katika kata ya Elerai ni:
NA
|
UGONJWA
|
AINA YA MIFUGO
|
PATWA
|
TIBIWA
|
KUFA
|
PONA
|
DAWA ILIYOTUMIKA
|
|
NDIGANA BARIDI
|
Ng’ombe
|
5
|
5
|
-
|
5
|
O.T.C 10%
Multivitamin |
|
HOMA YA KIWELE
|
Ng’ombe
|
2
|
2
|
-
|
2
|
Peniallon
|
|
NAGANA/NDOROBO
|
Ng’ombe
|
1
|
1
|
-
|
1
|
Novidium
O.T.C 10% |
|
MINYOO
|
Ng’ombe
Mbuzi |
3
19 |
3
19 |
-
|
3
19 |
Albendazole 10%
|
CHANJO KWA MIFUGO:
Hakuna chanjo yoyote kwa mifugo iliyotolewa.
HUDUMA NYINGINEZO (HUSBANDRY PRACTICES).
AINA YA MIFUGO |
IDADI |
HATUA |
NJIA ILIYOTUMIKA |
USHAURI |
MBUZI
|
2
|
Kukata pembe
|
Msumeno
|
Kurekebisha mifugo
|
NG’OMBE
|
1
|
kuhasi
|
Burdizo
|
Kuboresha mifugo
|
MBWA WAZURURAJI:
Mbwa wapatao 48 wameuwawa katika mtaa wa Kware na zoezi hili ni endelevu.
CHANGAMOTO NA MAFANIKIO
8:1: CHANGAMOTO:
Gharama za pembejeo za kilimo na mifugo kuwa juu.
Wafugaji wengi hufuga kwa mazoea/uzoefu.
8:2: MAFANIKIO:
Wafugaji wapatao watano (5) kunufaika na Elimu juu ya ufugaji bora na wenye tija.
MIRADI ILIYOIBULIWA.
ELIMU:
Kupatiwa jengo la Utawala kwa shule ya Elerai sekondari, Azimio s/msingi na Elerai s/msingi.
Kunahitajika matundu ya vyoo kama ifuatavyo:
i) Elerai s/msingi - matundu 70
ii) Azimio s/msingi matundu 27
iii) Burka s/msingi - matundu 29
iv) Elerai Sek - matundu 40
Vyumba vya madarasa.
i) Elerai s/msingi - vyumba 22
ii) Azimio s/msingi vyumba 08
iii) Burka s/msingi - vyumba 04
iv) Elerai Sek - vyumba 07
HUDUMA ZA JAMII
i) Barabara inayotoka kibaoni hadi TANAPA ipitishwe greda na kuweka vifusi
ii) Barabara ya mwisho wa hiace (stendi) ipanuliwe kwani ajali zimekuwa nyingi na gari kubwa inapita kwa tabu.
iii) Barabara ya kutoka TANAPA hadi Arusha meat itengenezwe kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa magari makubwa.
iv) Ofisi ya Kata ya Elerai igeuzwe kuwa sehemu ya kulaza wagonjwa na jengo lililopembeni ya ofisi ya kata ili kuwa ofisi ya kata /likarabatiwe..
v) Eneo la mgodini liandaliwe kwa ajili ya soko la mahindi ili lisikae bila faida.
vi) Barabara ya Tarimo mtaa wa Burka ifunguliwe upya na kujazwa vifusi inayoungana na Sakina.
vii) Matengenezo ya barabara ya kuansia kanisani hadi mabanzini kwa kuwekea vifusi.
viii) Kuwekwa mitaro ya maji kwa bara bara ya shamsi kibanda maziwa.
ix) Eneo la stendi majengo juu kupatikane vyoo vya kulipia.
x) Uhitaji wa viwanja vya michezo (kuna eneo linalouzwa mtaa wa URUNDINI na linafaa kugeuzwa kuwa kiwanja cha michezo).
xi) Mkandarasi wa taka, taka zimemzidi.
xii) Kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala/madarasa ya Elerai sekondari.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa