•Katika halmashauri ya Jiji la Arusha kuna shule za msingi 115 ikiwa za Serikali ni 46 na za binafsi ni 69.
•Halmashauri ina jumla ya wanafunzi wanaosoma katika shule za Serikali 55,412 ambapo wakiume ni 27,473 na wakike ni 27,939 na wanafundishwa na walimu 1529 kati yao wanaume ni 230 na wanawake ni 1299
•Katika kipindi hiki idadi ya walimu imeongezeka hadi kufikia walimu 2,184. Walimu hawa wanafundisha shule za msingi za serikali na za binafsi.
•Kitaaluma Elimu Msingi inafanya Vizuri kwani kwa mwaka 2016, Jiji la Arusha liliongoza Kimkoa na kuwa 5 Kitaifa katika Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi ambapo wanafunzi 7919 walifaulu kati yao 4129 ni wasichana 3790 ni wavulana, kiwango cha ufaulu ni sawa na asilimia 87.1.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa