TAARIFA YA KATA YA SAKINA
A: UTANGULIZI
Kata ya Sakina ni miongoni mwa kata 25 zilizopo katika jiji la Arusha. Pia Kata ya Sakina ni kata mpya iliyotokana na kugawanywa kwa kata ya Elelai na Ngarenaro. Ambapo kata hii ina jumla ya watu 21,988 wanawake wakiwa ni 11,572 na wanaume ni 10,416 na jumla ya kaya ni 6,921 ikiwa na jumla ya mitaa saba( 7)
MIPAKA YA KATA
kasikazini imepakana na Wilaya ya Arudha DC, kusini imepakana nan a kata ya sombetini na ungalimited kwa mitaa ya ostabay kwenye barabara ya Dodoma,Mashariki imepakana na kata ya Ngarenaro kwa mto N garenaro na magaribi imepakana na kata ya Eleraikwa barabara ya Shamsi hadi mto Rajabu kuendelea hadi mita 200.
WATUMISHI NA VIONGOZI
Ofisi ya kata ina jumla ya watumishi nane ( 8 ) nao ni kama ifuatavyo
VIONGOZI
2.0 HALI YA UTAWALA BORA KATIKA KATA
2. 1 MITAA ILIYOKO NDANI YA KATA YA SAKINA
KATA
|
MITAA
|
|
WAKAZI WALIOPO SENSA 2012
|
||||
SAKINA
|
7
|
|
MITAA
|
ME
|
KE
|
JUMLA
|
KAYA
|
|
|
SAKINA
|
1602
|
1705
|
3307
|
829
|
|
MELAMALI
|
1189
|
1290
|
2479
|
643
|
|||
MAIRIVA
|
1117
|
1320
|
2437
|
250
|
|||
NAVARANA
|
1981
|
1993
|
3974
|
1110
|
|||
GIRIKI
|
2116
|
2141
|
4257
|
1147
|
|||
OLMATEJO “A”
|
2583
|
2615
|
5198
|
1254
|
|||
OLMATEJO “B”
|
3223
|
3366
|
6586
|
1998
|
Jumla ya wakazi 28,241
Kutokana na kata ya sakina kua ni kata mpya hivyo kata yetu haijatengwa maeneo ya wazi hivyo kata haina shule za awali, msingi na sekondari, Zahanati pamoja na vituo vya afya vya serikali. Pia kata ya sakina haina taasisi za serikali.
MIRADI YA MAENDELEO
S/N
|
JINA LA MRADI
|
UTEKELEZAJI WA MRADI
|
MTEKELEZAJI
|
HALI YA MRADI KWA SASA
|
1
|
KUJAZA NA KUSHINDILIA VIFUSI KATIKA BARABARA YA GIRIKI
|
BARABARA IMEJAZWA NA KUSHINDILIWA KIFUSI
|
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
|
UMEMARIZIKA
|
2
|
UJENZI WA MTARO NA UMWAGAJI WA KIFUSI KATIKA BARABARA YA OLMATEJO B
(MSHENGERII) |
BARABARA PAMOJA NA MTARO KAKATIKA ENEO LA OLMATEJO B UMETENGENEZWA KWA UPANDE WA MTARO HAUJAKAMILIKA
|
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
|
UJENZI UNAENDELEA
|
MIPANGO YA KATA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA
Ushirikishaji Wananchi katika kupanga na kutekeleza mipango yao wenyewe,Ushirikishwaji Wananchi unazofaida nyingi ambazo ni pamoja na Wananchi kumiliki maendeleo yao; Miradi inayotekelezwa kuwa endelevu; Kuongezeka kwa uwajibikaji wa Wananchi na Viongozi wa Serikali za mitaa, pia Kuongezeka kwa uwazi katika kutoa maamuzi; Kupungua kwa gharama za Serikali za kutoa huduma kwa Wananchi kutokana na michango yao katika utekelezaji wa miradi; na kwa mujibu wa Ibara za 145 na 146 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ushirikishwaji wa Wananchi unalenga kutoa madaraka zaidi kwa Umma katika maamuzi.
Aidha, kujenga mazingira yanayowezesha Serikali na wananchi kushirikiana kuboresha utendaji wa kazi kwa upande wao na Serikali za Mitaa na kuhakikisha uwepo wa demokrasia ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.
DHANA: Kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa Jamii juu ya mpango shirikishi, Faida za kuwa na mpango shirikishi, na umuhimu wa kuunganisha nguvu kazi katika maendeleo. Pia kusisitiza uwajibikaji wa viongozi wa Jamii na Jamii yenyewe kwa ujumla katika suala zima la mchakato wa mipango.
Kuhakikisha kufuata kanuni ili kutomgandamiza mwananchi,pia kamati ya afya imeweka ratiba ya kutoa elimu ya afya kwa wananchi kwa kupitia mikutano ya mitaa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa