•Elimu ya Sekondari Jiji la Arusha lina jumla ya Shule 53 kati ya hizo 25 ni za Serikali na 28 ni binafsi/ Mashirika ya dini. Aidha Halmashauri ina Walimu 954, kati yao walimu 229 ni sayansi na 725 ni walimu wa sanaa na biashara. Halmashauri yetu ina wanafunzi 24,379, wakiume ni 11,586 na wakike ni 12,793.
•Katika mwaka wa Fedha 2014/2015 halmashauri imefanikiwa kujenga na kukamilisha maabara 62 zilizoligharimu jumla ya Tsh Bilioni 2.6 na Tsh Bil 2.5 ni mapato ya ndani wakati Mili 219.2 ni Fedha za CBG.
•Halmashauri pia imefanikiwa kuanzisha shule ya sekondari ya wasichana ya kidato cha tano kwa mchepuo wa Sayansi.
•Pamoja na hayo upanuzi wa Elimu ya Sekondari unakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maeneo kutokana na uhaba wa ardhi. Suala hili tunakabiliana nalo kwa kujenga shule za Maghorofa kwa kutumia mapato ya ndani.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa