IDARA YA UJENZI
Idara ya Ujenzi inafanya kazi chini ya sehemu ya Majengo, Barabara, Taa za barabarani,Karakana na umeme pamoja na Maji .
Sehemu hizi zinafanya kazi zifuatazo:
•Uratibu wa utoaji wa vibali vya ujenzi
•Usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya serikali kama Hospitali, Shule Ofisi za utawala , Vituo vya mabasi, Majengo ya biashara na uwekezaji, Usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya watu binafsi na kutoa ushauri, usanifu na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
•Kujenga Miundombinu ya barabara na vivuko ili kupitika mwaka mzima
•Kutengeneza barabara ili kupitika mwaka mzima
•Kukarabati Miundombinu ya barabara na vivuko ili kupitika mwaka mzima
•Kukarabati barabara ili kupitika mwaka mzima
UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi mjini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.
UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
•Kutimiza takwa la sheria ndogo za jiji
•Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji wa jiji
•Kudhibiti ujengo holela
TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
•Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na halmashauri ya jiji la Arusha yaabi “Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;
•Mkaguzi wa Majengo wa Jiji (Building Inspector)
•Afisa Ardhi wa Jiji (City land officer)
•Mpima wa Jiji (City Land surveyor)
•Afisa Mipango Miji wa Jiji (City Town Planning Officer)
•Afisa Afya wa Jiji (City Health and Sanitation Officer)
•Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “architectural & structural drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo;
i.Mkaguzi wa Majengo wa Jiji (Building inspector) - kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications
ii.Afisa Ardhi wa Jiji (City land officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.
iii.Mpima wa Jiji (City Land Surveyor) – kutambua mipaka halali
iv.Afisa Mipango Miji wa Jiji (City Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji, eneo la maegesho lipo, nk
v.Afisa Afya wa Jiji (City Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyema
•Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali
•Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya benki 40801200336 - “council own source collection”
•Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na afisa mipango miji
MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI
•Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili (2) hadi manne (4)
•Hii ni pamoja na kuwasilishaji wa ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.
WAJIBU WA MWANANCHI
•Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya jiji kwa kibali kutoka jiji la Arusha
•Wakazi wote wa katikati ya mji “CBD” wanapaswa kukarabati au kujenga nyumba za kwenda juu (maghorofa) tu.
•Hairuhusiwi kujenga au kukarabati nyumba za chini
TAHADHARI
•Endapo mwananchi yoyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka jiji la Arusha, atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba (4)
•Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha, jiji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa jiji litabomoa kjengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji huo
•Wananchi wote wa Jiji la Arusha wanashauriwa kuacha ujenzi holela kwa kufuata sheria ndogo za ujenzi na kupata kibali cha ujenzi
USIMAMIZI WA UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SERIKALI
Jukumu la msingi la Idara hii ni kusimamia ujenzi na ukarabati wa majengo ya yote serikali yaliyoko chini ya Halmashauti ya Jiji;
Jiji limeandaa fomu za kujaza zinazoainisha hatua za ujenzi kama ifuatavyo, Nyumba za chini Setting out, Kuchimba msingi , Kuweka blinding, Kujenga msingi ikiwa ni pamoja na kweka nondo stahili , Kupanga mawe ,Kumwaga zege la msingi na Kukagua na kujenga msingi wa matofali au mawe.
Hatua zingine za zilizoainishwa ni Kuweka ring beam la chini, Kujaza msingi kutumia udongo stahili, Kewaka na kupanga mawe”hadcore”, Kuweka DPM, Kuweka jamvi, Kujenga kuta kwa matofali, Kuweka ring beam, Kusuka na kujenga paa, Kuweka /kupiga bati, Kuweka frame, Kuweka mabomba ya umeme (conduit pipes) pamoja na Kufanya/kuweka plaster.
Kuweka mbao za ceiling “brandering” na kufunika “plain sheets”, Kuweka sakafu , Kufanya majaribio ya mfumo wa umeme, Kufanya mfumo wa maji safi na taka, bomba za maji taka na maji safi, mashimo yote soak away/ cessipit pit, septic, manholes na inspection chambers, Kufanya majaribio ya mfumo wa maji taka na safi , Kufanya mfumo wa umeme – wiring, kuweka vifaa sockets, switches, tube lights, lumps, Kupiga rangi ndani na nje , Kufanya usafi ndani na nje ya jengo na Kukabidhi site kwa matumizi pia zimeainishwa katika Fomu hizo.
Majengo yote ya Serikali yanapojengwa ni lazima yakaguliwa katika kila hatua ya ujezi pia kuna fomu za kujaza zinazoainisha hatua mbalimbali za ukaguzi. Fomu hizi lazima zijazwe na wataalamu washauri na kuwasilishwa ofisi za jiji kwa ukaguzi.
Jiji linakagua kila hatua ya ujenzi na kuidhinishana na Jiji linapaswa kupata ilani ya masaa arobaini na nane (48) kwa ajili ya ukaguzi wa kila hatua.
USHAURI NA USANIFU NA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU
Idara ya Ujenzi inatoa huduma za ushauri na usanifu wa ujenzi wa gharama nafuu pia Ushauri wa teknolojia za utengenezaji wa vifaa vya ujenzi. Huduma zingine ni kama usanifu wa majengo (structural) pamoja na uandaaji wa gharama za ujenzi (Bills of Quantities - BOQs).
CHANGAMOTO YA SEHEMU ZA BARABARA
•Uhitaji wa barabara kuwa mkubwa ambapo hauendani na kiasi cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara.
•Wizi na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
•Barabara za udongo na changarawe kuharibiwa na mvua hivyo kuhitaji kufanyiwa matengenezo mara kwa mara.
•Uvamizi wa maeneo ya hifadhi barabara unaofanywa na watu hivyo kufanya kazi za matengenezo ya barabara ya mifereji kwa ngumu.
•Utupaji wa taka ngumu kwenye mifereji ya maji ya mvua ambapo husababisha maji kushindwa kupita kirahisi.
MIKAKATI YA KUBORESHA BARABARA
•Kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwani kwa sasa Halmashauri inategemea vyanzo viwili tu ambavyo ni makusanyo ya ndani na Mfuko wa Barabara.
•Kuelimisha jamii umuhimu wa kushiriki kulinda miundombinu ya barabara isiibiwe kwani waathirika wakubwa ni jamii nzima.
•Kuelimisha Jamii kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi ya barabara.
•Kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waache kutupa takataka ngumu kwenye mifereji ya maji ya mvua
WITO
Wananchi wote wanatakiwa kuzitunza barabara kwa maendeleo endelevu. Mkulima, mfugaji na mfanyabiashara hakikisha unaweka akiba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba bora na ya kisasa (Maisha ni nyumba).
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa