UTANGULIZI
Idara ya maendeleo na ustawi wa Jamii ina vitengo sita ambavyo kwa pamoja vinatekeleza majukumu yafuatayo:
SHUGHULI ZA MAENDELEO
•Kuhamasisha Jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ya sekta ya mbalimbali ikiwa ni sekta ya Kilimo Mifugo, Afya, Elimu na Maji
•kuwezesha Jamii kushiriki katika hatua ya kupanga, kuibua na kusimamia miradi kupitia mikutano na vikao ngazi ya mitaa, na kata.
UKIMWI
Katika jiji la Arusha hali halisi ya maambukizi ya VVU/ Ukimwi yanaonyesha kupungua kutoka asilimia 3.1 hadi 2.2 Idara inaendelea kutekeleza shughuli zifuatazo katika kudhibiti maambukizi ya VVU kama ifuatavyo:
•Kutoa mafunzo ya kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa vikundi, Vicoba na Sacoos ili familia kujiwekea akiba.
•Kuhamasisha WAVIU (watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi)kujiunga kwenye vikundi, Saccos, na Vicoba kwa wanawake kwa ajili ya kujiongezea kipato ngazi ya familia.
•Kutoa msaada kwa watoto yatima waliotambuliwa ngazi ya Kata na mtaa husika Katika masuala ya Elimu kwa kuwalipia ada, na sare.
•Kutoa kielimu katika masuala ya ujasiriamali kwa vikundi, Saccos na Vicoba vya WAVIU (watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi)
•Kutoa ushauri nasaha na upimaji wa afya kwa hiari kwa Jamii ili kujua afya zao.
UTAFITI NA MIPANGO
•Kutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala ya uanzishaji na uendeshaji wa NGOS, CBOs, na FBOS zinazoto huduma kwa Jamii kwa ujumla
•Kutoa elimu kwa Jamii juu ya ushirikishwaji katika hatua ya kupanga, kuibua, kutekeleza, kufuatilia na kufanya tathimini ya miradi ya kilimo na ufugaji
•Kutoa ushauri na elimu ya ujasiriamali kwa Jamii katika masuala ya utunzaji wa kumbukumbu, huduma kwa wateja
WANAWAKE, JINSIA NA WATOTO
Kuwezesha wanawake kiuchumi,
•Kuwezesha Jamii kuunda na kusajili vikundi, Saccos na Vicoba kwa wanawake ili kuweza kukopesheka na taasisi za kifedha pamoja na halmashauri kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake hatimaye kurahisisha Urejeshaji wa Mikopo hiyo.
•Kusimamia haki za watoto ngazi ya familia kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009
•Kusimamia na kutetea haki za wanawake kwa kuzingatia dhana ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za maamuzi.
MAENDELEO YA VIJANA
Kuwezesha vijana kiuchumi
•Kuwezesha na kutoa elimu ya uundaji na usajili wa vikundi na Saccos kwa vijana ili kuweza kukopesheka na tasisi za kifedha pamoja na halmashauri kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana na hatimaye kurahisisha Urejeshaji wa Mikopo hiyo.
•kutoa ushauri wa kitaalamu kwa vijana katika masuala ya afya ya msingi, stadi za kazi, malezi na makuzi
MFUKO WA AFYA YA JAMII-TIBA KWA KADI (TIKA)
Ni mpango wa hiari unaoiwezesha jamii kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia mara moja tu kiasi cha fedha kwa kadiri jamii yenyewe katika Halmashauri husika itakavyoamua. Katika Jiji la Arusha kiasi cha uchangiaji ni Tsh. 12,000 kwa kaya yenye Baba , mama na wategemezi wanne waliochini ya miaka 18, mtu mmoja moja, wanafunzi sita katika kundi moja. Mpango huu unalenga wakulima na wafugaji,wavuvi,wajasiriamali,vikundi vya uzalishalishaji mali na tasisi.
Aidha Idara ya Maendeleo ya jamii inaendelea na kuratibu na kuhamasisha jamii kujiunga na mpango wa Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa ajili ya kupata huduma ya Afya kwa gharama nafuu na kutoa maelekezo ya vituo vya kutolea huduma ya Afya
MPANGO WA LISHE
•Kuhamasisha jamii kuhusiana na umuhimu wa lishe bora sambamba na umuhimu wa upimaji wa afya mara kwa mara ili kujua hali zao za afya hasa lishe.
•Kuhamasisha Jamii na kusimamia uanzishaji wa bustani za nyumbani kwa ajili ya kuboresha lishe ya familia.
MAJUKUMU YA USTAWI WA JAMII
(i)HUDUMA KWA FAMILIA, WATOTO NA MALEZI YA AWALI YA MTOTO
Kitengo hiki kinatoa huduma zake kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na sheria zifuatazo:
•Sheria ya Ndoa Na. 5 ya mwaka 1971;
•Sheria ya mtoto ya mwaka 2009;
•Sheria ya kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ‘’The Anti-Trafficking in Persons’’ Act, 2008
Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-
Huduma za usuluhishi wa ndoa zenye mifarakano;
Huduma ya matunzo kwa watoto walio kwenye ndoa zenye mfarakano;
Huduma ya matunzo kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa;
Huduma ya makao ya kulelea watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi;
Huduma ya malezi ya kambo na kuasili
Huduma ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo.
Huduma ya Malezi, Matunzo na Ulinzi shirikishi Jamii kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi (community based care, support and protection of orphans and vulnerable children
Huduma kwa familia zenye dhiki
(ii) MAREKEBISHO YA TABIA NA HAKI ZA MTOTO KISHERIA:
Kitengo hiki kinatoa huduma kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na Sheria mbalimbali. Sheria hizo ni;
•Sheria ya mtoto ya mwaka 2009
•Sheria ya Huduma za Majaribio na Ujenzi wa Tabia (Sura Na.247)
•Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Na.4 ya Mwaka 1998
•Sheria ya Kanuni za adhabu (Sura ya 16)
•Sheria ya Huduma kwa jamii Na.6 ya Mwaka 2002
Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-
Haki za watoto/vijana (Juvenile Justice
Huduma katika Mahabusi za watoto
Huduma za shule ya maadilisho
Huduma kwa watoto watukutu (Juvenile delinquents)
Huduma zitolewazo katika Mahakama ya watoto
Huduma kwa watoto wanaoishi mitaani
Huduma ya elimu juu ya athari ya pombe na madawa ya kulevya
(ii) HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU NA WAZEE:
Kitengo hiki kinatoa huduma kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na Sheria zifuatazo:
Sera:
•Sera ya Taifa ya Wazee (2003);
•Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu (2004).
Sheria:
•Sheria ya Watu Wenye Ulemavu (Na. 9, ya 2010)
Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-
Mafunzo ya Stadi za kazi kwa watumishi wa Ulemavu:
Utengemao kwa Watu wenye Ulemavu:
Marekebisho
Matunzo kwa Watu wenye Ulemavu/Wasiojiweza:
Huduma ya Utengemao kwa wazee walio katika makazi:
Huduma za ushauri kwa Wazee:
Nyenzo za Kujimudu:
Huduma kwa Vyama/Asasi za Watu wenye Ulemavu:
(ii) PROGRAMU ZINAZOSIMAMIWA NA IDARA YA USTAWI WA JAMII
Mpango shirikishi jamii wa malezi, matunzo na ulinzi kwa yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi
Mpango wa Uwezeshaji Haki Jamii
Programu ya stadi za malezi ya watoto walio katika mazingira hatarishi
Programu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo 0-8
Mpango wa Uzuiaji Usafirishaji Haramu wa Watu
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa