Tangu kuanzishwa kwa Halmashospitali moja tuu ya M hospitali ya Wilaya. Kwa sasa tuna hospitali 5. Aidha hapakuwa na Kituo cha Afya katika Wilaya, ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo kuna Vituo (14) ambapo 7 ni vya Serikali na 7 vinamilikiwa na mashirika na watu binafsi. Zahanati zipo 60 kati ya hizo 6 ni Serikali, 52 ni Binafsi na 5 zipo katika hatua za Ujenzi .
Katika sekta ya Afya tunayo kazi kubwa ya kupambana na magonjwa yote hasa Malaria na HIV/AIDs, kwa kuzingatia hali duni ya mapato ya watanzania walio wengi na kuibuka kwa magonjwa yasiyoambukizwa kama vile Kansa, Magonjwa ya moyo na Kisukari.
Jukumu lililoko mbele yetu ni kuhakikisha, wakazi wote hasa wale wenye kipato cha chini wanapata huduma ya kuridhisha na Elimu ya Afya ya Msingi. Aidha tunao wajibu wa kuzingatia zaidi suala la kinga ya magonjwa kuliko kusubiri tiba.Ili kutekeleza majukumu haya masuala muhimu yafuatayo hayana budi kuzingatiwa:-
•Kuanzisha programu maalum za kusaidia wakazi wenye kipato cha chini, ili waweze kupata huduma nzuri za afya.
•Kuendelea kutoa Elimu ya Afya ya Msingi kwa wananchi wote ili kupunguza magonjwa yanayozuilika.
•Kuendela kuwashawishi watu binafsi kutoa huduma za afya kwa gharama nafuu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa