Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni ametoa Shilingi Milioni 1 kama asante kwa wafanyabiashara watano wa Soko Kuu ambao Walilazimishwa kulipa ushuru wa Shilingi 500 huku wakiwa
na vitambushulisho vya kuwatambua kama waasiriamali wadogo
Wakati akitoa fedha hizo leo Tarehe 02 Machi,2019 Dkt. Madeni amesema kuwa fedha hizo amezitoa katika mshahara wake kwa ajili ya kuwaongezea mitaji wafanyabiashara hao ili kuwainua kiuchumia pamoja na kuwapa pole kufuatia adha waliyokumbana nayo yakulazimishwa kutoa ushuruwa Sh. 500 na Mkuu wa Soko la hilo, Yusuf Ngenya iliyotokea siku ya
Jumatano Tarehe 27 Februari mwaka huu
“Natoa fedha hizi kuwafariji kutokana na kitendo alichokifanya Mkuu wa Soko kuu kuwatoza ushuru ilhali akijua kuwa mnavyo vitambulisho vinavypwatambua kama wajasiriamali wadogo almaarufu kama machinga” alisema Dkt. Madeni.
“Kitendo kilichofanywa na mtumishi aliyechini yangu kimesababisha kuwaweka wafanyabiashara hawa katika huzuni hali ya kuwa wanaishi katika Nchi huru na wanavyo vitambulisho vya kuwatambua kama wajasiriamali wadogo na pia namuomba Radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kitendo kile alichokifanya kuwatoza ushuru
kinamama hawa huku akijua ni kiyume na maelekezo ya Rais wetu mpendwa”. Aliongeza Dkt. Madeni.
Naye Bi. Dorah Patric mmoja kati ya wafanyabiashara waliokumbwa nakadhia hiyo alishukuru kupata fedha hizo kwani mtaji wake wa machungwa ni Sh.15,000 hivyo kitendo cha kupewa Sh.200,000 na Mkurugenzi wa Jiji kitamsaidia kukuza biashara yake .
“Ukweli Namshukuru Mungu kwani sijategemea kupata fedha hizi. Namshukuru Mkurugenzi wetu kwa kunipa hela hii kutokana na ujasiriwangu wa kugoma kulipa sh. 500 wakati ninakitambulisho”. alisema Dorah
Awali aliyekuwa Mkuu wa Soko hilo, Yusuf Ngenyaambaye pia kwa sasa ameondolewa katika nafasi hiyo kwa kushindwa kufikiamalengo ya ukusanyaji wamapato ndani ya soko hilo alipopewa nafasi ya kujitetea mbele yaMkurugenzi Dkt. Madeni alisema kuwa aliamua kurekodi video wakati akidaiushuru kwa wafanyabiashara hao kamaushahidi wakati atakapokuja kuulizwa sababu za mapato ya soko kushuka na video hiyo pia iweze kuonyesha jinsiwafanyabiashara wanavyogoma kulia ushuru wa masoko.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa