Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Arusha Ndg.Msena Bina amezungumza na waandishi wa habari juu ya uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema tarehe 24 Novemba mwaka huu .
Akizungumza na waandishi hao Ndg.Msena amesema katika kipindi hiki cha kampeni kuanzia Tarehe 17-23 Novemba 2019 wananchi wajitokeze kwa wingi kusikiliza sera za wagombea wao kwani kiongozi mzuri ndiye atakayeleta maendeleo katika Mtaa wake kwa kuibua miradi na kupeleka katika ngazi husika
Katika Halmashauri ya Jiji la Arusha vyama vilivyobaki ni viwili ambavyo ni Chama cha Mapinduzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo hivyo jumla ya kata zitakazoshiriki uchaguzi huo ni kata 7 yenye jumla ya Mitaa 15. Kata hizo ni pamoja na Kata ya Moshono Mtaa wa Losirwai, Kata ya Olmoti Mitaa ni Ngaramtoni ya chini, Olmot na Olteves , Kata ya Sinoni Mtaa ni Onjavutiyan, Makao mapya na Olmokea , Kata ya Lemara Mitaa ni Kikokwaru B, Olepolos, Ilkirowa na Sun flag, Kata ya Sombetini ni Mtaa mmoja wa Banda mbili, Kata ya Daraja II Mtaa wa Sanare na Darajani na Kata ya Unga ltd Mtaa wa Tindigani.
Aidha Ndg. Msena Bina ameeleza kuwa nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti wa Mtaa/Kijiji nafasi 3, wajumbe mchanganyiko nafasi 10 pamoja na wajumbe wanawake[viti maaluM] nafasi 8.
Hivyo jumla ya mitaa katika Hamashauri nzima ni 154 kati ya hiyo ni mitaa 151 ndiyo iliyopita bila kupingwa kwa Nafasi ya mwenyekiti. Ndg.Msena ameendele kusema kuwa katika uchaguzi huu haki imetendeka na kanuni za uchaguzi zimefuatwa hivyo uchaguzi ni wa huru na haki.
Mwisho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa